Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa wabunge na urais unafanyika nchini Sierra Leone

Nairobi – Raia nchini Sierra Leone wanapiga kura kuwachagua wabunge wapya na rais, uchaguzi unaotajwa kuwa wenye ushindani mkali haswa wakati huu taifa hilo linalokabiliwa na mzozo wa gharama za maisha.

Raia nchini Sierra Leone wanapiga kura
Raia nchini Sierra Leone wanapiga kura REUTERS - COOPER INVEEN
Matangazo ya kibiashara

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kuchelewa kinyume na iliyopangwa katika mji mkuu, Freetown, ambapo zoezi hilo liliaanza saa moja asubuhi na linatarajiwa kukamilika saa moja jioni.

Takriban watu milioni 3.4 wamejiandikisha kupiga kura, asilimia 52.4 kati yao wakiwa na umri wa chini ya miaka 35, kulingana na msemaji wa tume ya uchaguzi.

Wagombea 13 wanawania wadhifa wa urais, ikiwa ni pamoja na Julius Maada Bio, Uchaguzi unaofanyika wakati huu kukiwa na mzozo wa kiuchumi uliodorora, hali iliyosababisha kutokea kwa ghasia mbaya mwaka jana.

Freetown, Sierra Leone
Freetown, Sierra Leone © AFP

Mgombea  urais anahitajika kupata asilimia 55 ya kura halali ilikutangazwa mshindi katika duru ya kwanza.

Mpinzani mkuu wa Bio aliye madarakani ni Samura Kamara wa chama cha All People's Congress (APC).

Bio, 59, wa Chama cha Sierra Leone People’s Party (SLPP), alimshinda Kamara, ambaye mwenye umri wa miaka 72, katika duru ya pili ya uchaguzi mwaka 2018.

Mfumuko wa bei wa mwaka hadi mwaka ulifikia asilimia 43 mwezi Aprili, kulingana na takwimu rasmi za hivi punde.

Idadi kubwa ya raia nchini Sierra Leone wanakabiliwa na tatizo la umaskini
Idadi kubwa ya raia nchini Sierra Leone wanakabiliwa na tatizo la umaskini © JOHN WESSELS / AFP

Wote wawili Bio na Kamara waliiambia AFP wangeweka kipaumbele katika kukuza uzalishaji wa kilimo.

Taifa hilo maskini sana la Afrika Magharibi lilikumbwa na vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vya 1991-2002 na janga la Ebola muongo mmoja baadaye, na kuathiriwa zaidi kiuchumi na janga la uviko 19 pamoja na mapigano nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.