Pata taarifa kuu

Sierra Leone: Kila pande zadai kushinda katika uchaguzi wa urais

Shughuli ya kujumlisha matokeo ya kura inaendelea nchini Sierra Leone siku mbili baada ya uchaguzi mkuu kufanyika.

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini humo
Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini humo REUTERS - COOPER INVEEN
Matangazo ya kibiashara

Haijabainika ni nani anaongoza katika kinyang'anyiro cha urais kati ya Rais Julius Maada Bio na mshindani wake mkuu Samura Kamara, lakini pande zote mbili tayari zimesema zimeshinda uchaguzi huo.

Waangalizi wa uchaguzi wamewataka raia nchini humo na wagombea hao kuwa watulivu na kusubiri matokeo rasmi.

Licha ya wito huo kutoka kwa tume ya uchaguzi kuna wasiwasi kutokana na hatua ya tume kutoaanza kutangaza matokeo ya awali.  

Ujumbe wa Umoja wa Ulaya uliitaka tume ya uchaguzi kutoa "uwazi kamili wakati wa uwasilishaji wa matokeo" ili kupunguza mvutano.

Kituo cha Carter pia kilielezea wasiwasi wake juu ya "ripoti zinazoonyesha kukosekana kwa uwazi wakati wa mchakato wa kujumlisha matokeo ya uchaguzi huo

Mshindi wa uchaguzi huo lazima apate asilimia 55 ya kura halali zilizopigwa, la sivyo kutakuwa na duru ya pili kati ya wagombea wawili wa juu wiki mbili baada ya kutangazwa kwa matokeo.

Mengi yako hatarini wakati nchi hiyo ya Afrika Magharibi inakabiliwa na masuala mengi ikiwa ni pamoja na hali mbaya ya gharama ya maisha, umaskini na ukosefu mkubwa wa ajira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.