Pata taarifa kuu

Sierra Leone: Polisi wamezingira makao makuu ya chama cha upinzani

Wanajeshi wamezingira makao makuu ya chama kikuu cha upinzani nchini Sierra Leone, huku kura zikihesabiwa katika uchaguzi wa urais uliofanyika nchini humo.

Samura Kamara, kiongozi wa upinzani nchini Sierra Leone
Samura Kamara, kiongozi wa upinzani nchini Sierra Leone AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mgombea mkuu wa upinzani Samura Kamara kupitia ukurasa wake wa Twitter, amedai kuwa risasi ilifwatuliwa ndani ya ofisi yake huku kukiwa na ripoti kuwa mwanamke mmoja alipoteza maisha.

 

 

Kiongozi huyo wa chama cha  All People's Congress, Samura Kamara, amesema tukio hilo ni sawa na jaribio la mauaji.

Waangalizi wa Kimataifa wameonesha wasiwasi wao kuhusu muda mrefu unaotumiwa kujumuisha matokeo ya urais.

Haijabainika ni kwa nini  wanajeshi ilitumwa katika eneo hilo, swala ambalo maofisa wa polisi bado hawajazungumzia.

 

 

Upinzani nchini humo unatarajia kumuondoa madarakani rais Julius Maada Bio, ambaye anawania kwa muhula wa pili.

Kulikuwa na ghasia za hapa na pale dhidi ya maafisa wa uchaguzi wakati wa upigaji kura siku ya Jumamosi baada ya kampeni za mvutano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.