Pata taarifa kuu

Sierra Leone : Rais Julius Maada Bio ameapishwa kuhudumu muhula wa pili

Nairobi – Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio ameapishwa kuhudumu muhula wake wa pili, baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi ambao mpinzani wake mkuu amesema haukuwa wa kuaminika.

Julius Maada Bio, ameapishwa kuongoza kwa muhula wa pili
Julius Maada Bio, ameapishwa kuongoza kwa muhula wa pili REUTERS - PHIL NOBLE
Matangazo ya kibiashara

Bio mwenye umri wa miaka 59, ameanza muhula wake wa pili kama rais wa taifa hilo ambalo limekuwa likikumbwa na changamoto tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya 1991-2002, ikiwemo ugonjwa ebola na uchumi unaodorora.

Kulingana na tume ya uchaguzi, rais Bio alipata ushindi wa asilimia 56 licha ya mpinzani wake mkuu Samura Kamara aliyemaliza wa pili kwa asilimia 41, kupinga matokeo hayo.

Siku ya Jumatatu, Chama cha kamara APC katika taarifa kilishtumu ukosefu wa uwazi na uwajibikaji kutokakwa tume ya uchaguzi, kutokana na kukosekana kwa taarifa kuhusu vituo au wilaya ambazo kura zilikuwa zikitoka.

Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu,Waangalizi wa umoja wa walisema kuwa ukosefu wa uwazi na mawasiliano kutokakwa tuma ya uchaguzi yalisababisha mchakato huo kutoaminika.

Kwa upande wake, Bio amesema amefurahishwa na ushindi Wake huku akielezea matamanio yake kufufa uchumi wa nchi na kutengeneza nafasi za ajira.

Kulingana na tume ya uchaguzi, asilimia 83 ya wapiga kura waliosajiliwa walijitokeza kushiriki kwenye uchaguzi huo wa Jumamosi iliopita Juni 24.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.