Pata taarifa kuu

Libya: Walanguzi wa binadamu 37 wamefungwa jela

Nairobi – Mahakama nchini Libya, imewafunga jela watu 37 waliohukumiwa kwa makosa ya ulanguzi wa binadamu kufuatia vifo vya wahamiaji 11 waliozama katika bahari ya Mediterranean.

Wahamiaji wengi kutoka bara Afrika wamekuwa wakitumia njia hatari kuvuka bahari kuelekea ulaya
Wahamiaji wengi kutoka bara Afrika wamekuwa wakitumia njia hatari kuvuka bahari kuelekea ulaya © Petros Karadjias / AP
Matangazo ya kibiashara

Wanachama watano wa kundi la kihalifu walifungwa jela maisha wakati wengine wakipewa kifungo cha kati yam waka moja hadi kumi na tano jela.

Kwa mujibu wa mahakama, watu hao walihusika katika upangaji wa kuwasafirisha wahamiaji kwenda nchini Italia kwa kutumia boti mbovu na hatari.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanaeeleza kwamba wahamiaji hukabiliwa unyanyasaji mikononi mwa walanguzi wa binadamu na hata kwenye vizuizi vya serikali.

Libya imekuwa ikikabiliwa na matatizo na machafuko tangu kuangushwa kwa utawala wa kanali Muammar Gaddafi mwaka wa 2011.

Idadi ya watu wanaofariki baada ya kuzama katika bahari ya Mediterranean wakitaka kuvuka kwenda kutafuta maisha bora Ulaya imeongezeka katika siku za hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.