Pata taarifa kuu

Putin hatahudhuria mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini

Nairobi – Rais wa Urusi Vladimir Putin hatahudhuria mkutano wa kilele wa mataifa ya BRICS nchini Afrika Kusini mwezi Agosti, ofisi ya rais wa nchi hiyo imesema , na hivyo kumaliza uvumi wa miezi kadhaa kwamba kiongozi huyo wa Urusi angehudhuria.

Afrika kusini imekuwa ikipokea shinikizo kutomualika mwenzake wa Urusi
Afrika kusini imekuwa ikipokea shinikizo kutomualika mwenzake wa Urusi via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya  rais Putin kuhuduria mkutano huo imeonekana kuwa changamoto kwa nchi ya Afrika Kusini haswa kuhusu suala la kidiplomasia.

Rais wa Urusi anayetakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, ambaye Afrika Kusini ni mwanachama, ina maana kuwa taifa hilo la Afrika linafaa kumkamata kwa mujibu wa sheria iwapo angeingia nchini humo.

Kwa mujibu wa msemaji wa rais wa Cyril Ramaphosa, hatua hiyo imeafikiwa baada ya kufanyika kwa makubaliano ya pande zote na kwamba Urusi itawakilishwa na waziri wake wa mambo ya kigeno Sergei Lavrov.

Rais wa Afrika Kusini ni mshirika wa karibu wa rais wa Urusi
Rais wa Afrika Kusini ni mshirika wa karibu wa rais wa Urusi via REUTERS - HOST PHOTO AGENCY RIA NOVOSTI

Afrika Kusini ni mwanachama wa muungano wa BRICS unaojumuisha mataifa ya Brazil, Urusi, India na China.

Putin alikuwa amealikwa kwenye mkutano huo wa BRICS unaotarajiwa kufanyika mjini Johannesburg kati ya Agosti 22 na 24 japokuwa  Pretoria imekuwa inakabiliwa na shinikizo kutoka ndani na nje ya nchi kutomualika.

Rais wa Urusi anatakiwa na ICC kutokana na madai kwamba Urusi iliwafukuza watoto raia wa Ukraine kinuyme na sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.