Pata taarifa kuu

Sudan: Watu 16 wameuwa katika shambulio la roketi jimboni Darfur

Nairobi – Watu 16 wameuwa jimboni Darfur nchini Sudan, baada ya kushambuliwa na roketi iliyolenga makaazi yao, wakati huu mapigano yakiendelea kati ya Jeshi na wanamgambo wa RSF. 

Wanajeshi wa serikali ya Sudan wamekuwa wakikabiliana na wapiganaji wa kikosi cha RSF kwa miezi kadhaa sasa
Wanajeshi wa serikali ya Sudan wamekuwa wakikabiliana na wapiganaji wa kikosi cha RSF kwa miezi kadhaa sasa AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa mawakili umesema shambulio hilo limetokea wakati wa makabiliano kati ya wanajeshi na wanamgambo wa RSF katika mji mkuu wa jimbo hilo Nyala. 

Mbali na mauaji hayo, watu wameendelea kuyakimbia makaazi yao, wakati huu maelfu wakikimbilia katika nchi jirani ya Chad kutokana na vita hivi ambavyo vimesababisha vifo vya watu Elfu tatu, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa. 

Mapigano yanayoendelea, yamekuwa yakilenga zaidi katika mji wa El Geneina, ambako Umoja wa Mataifa umeripoti mauaji makubwa ya raia, pamoja na visa vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu. 

Mauaji haya yanakuja siku chache tu baada ya kiongozi wa Mashtaka kwenye Mahakama ya Kimataifa ya ICC Karim Khan kutangaza kuwa Ofisi yake inachunguza ripoti ya kutokea kwa uhalifu wa livita katika jimboi la Darfur, baada ya miili ya watu 87 kutoka kabila la Masalit kukutwa katika kaburi la pamoja. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.