Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Jacob Zuma amerejea nyumbani akitokea Urusi

Nairobi – Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amerejea nchini humo akitokea nchini Urusi ambako alikuwa ameenda kupokea matibabu.

Zuma aliachiwa huru mwezi Septemba mwaka wa 2021 baada ya kuzuiliwa gerezani kwa kipindi cha wiki nane.
Zuma aliachiwa huru mwezi Septemba mwaka wa 2021 baada ya kuzuiliwa gerezani kwa kipindi cha wiki nane. AFP - EMMANUEL CROSET
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa wakfu wa kiongozi huyo wa zamani, matibabu yake na uchunguzi wa kiafya yalifanyika vizuri.

Ziara yake ilifanyika baada ya kupoteza rufa katika mahakama ya kikatiba mwezi uliopita ya kutaka kuzuia uamuzi wa kurejeshwa gerezani.

Mahakama ya kikatiba iliamua kwamba Zuma alikuwa amepewa ombi la kwenda kutafuta matibabu kinyume na sheria.

Idara ya magereza nchini humo sasa imempa kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 81 hadi Ijumaa kutotoa sababu ni kwa nini hafai kurejeshwa gerezani kumaliza kifungo chake cha miezi 15.

Zuma aliachiwa huru mwezi Septemba mwaka wa 2021 baada ya kuzuiliwa gerezani kwa kipindi cha wiki nane.

Alipewa ruhusa ya kuondoka gerezani na mkuu zamani wa idara ya magereza Arthur Fraser, ambaye ametajwa kuwa mtu wa karibu na Zuma.

Rais huyo wa zamani alikuwa amehukumiwa kwa makosa ya kudharau mahakama baada yake kukataa kutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi dhidi ya madai ya ufisadi wakati akiwa afisini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.