Pata taarifa kuu

Hatua ya serikali ya Misri ya kupiga marufuku niqab shuleni yazua mjadala

Wizara ya Elimu ya Misri imepiga marufuku uvaaji wa sitara kamili katika shule za umma na za kibinafsi, uamuzi ambao umezua mjadala siku ya Jumanne kwenye mitandao ya kijamii katika nchi hiyo ya Kiarabu yenye watu wengi zaidi.

"Watu wana hasira kwa sababu serikali haijatoa uhalali wowote, ni uamuzi wa kidhalimu ambao unaingilia maisha ya kibinafsi," anajibu Mohammed kwenye X (zamani ikiitwa Twitter). "Hakuna anayekasirika isipokuwa wale wanaounga mkono Taliban na Islamic State (IS)," anajibu "al-Masri" kwenye mtandao huo wa X.
"Watu wana hasira kwa sababu serikali haijatoa uhalali wowote, ni uamuzi wa kidhalimu ambao unaingilia maisha ya kibinafsi," anajibu Mohammed kwenye X (zamani ikiitwa Twitter). "Hakuna anayekasirika isipokuwa wale wanaounga mkono Taliban na Islamic State (IS)," anajibu "al-Masri" kwenye mtandao huo wa X. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu, Gazeti la serikali la Akhbar al-Youm lilichapisha agizo hilo mpya kuhusu sare za shule ambalo linakataza wanafunzi wa shule za msingi na upili "kufunika nyuso zao".

Sitara ni "hiari", inabainisha agizo, kulingana na "nia ya mwanafunzi, bila shinikizo au kulazimishwa kutoka kwa mtu yeyote isipokuwa mlezi wake kisheria, ambaye lazima ajulishwe juu ya uchaguzi huu". Ingawa wengi wa wanawake wa Misri huvaa hijabu, niqab bado ni wachache katika nchi hii yenye Waislamu wengi.

"Watu wana hasira kwa sababu serikali haijatoa uhalali wowote, ni uamuzi wa kidhalimu ambao unaingilia maisha ya kibinafsi," anajibu Mohammed kwenye X (zamani ikiitwa Twitter). "Hakuna anayekasirika isipokuwa wale wanaounga mkono Taliban na Islamic State (IS)," anajibu "al-Masri" kwenye mtandao huo wa X.

Tangu Bw. Sissi amuondoe madarakani rais Mohamed Morsi - mwanachama wa Muslim Brotherhood - mwaka 2013, udugu huo, uliotangazwa kuwa "kigaidi", umepigwa marufuku na wanachama na viongozi wake wameuawa na mamia kwa maelfu kufungwa jela.

Kwa watumiaji wa Intaneti, hata hivyo, tatizo la elimu katika nchi yenye wakazi milioni 105 waliokandamizwa na mfumuko wa bei na deni la umma liko kwingineko. "Je, ni niqabu ambayo inawajibika kwa madarasa yenye msongamano wa wanafunzi, kuchakaa kwa vifaa na matatizo ya walimu?", anauliza kwa kejeli mtumiaji mwingine wa mtandao.

Mwishoni mwa mwaka wa 2015, Chuo Kikuu cha Cairo, kimojawapo cha vyuo vikuu vikongwe na vyenye hadhi kubwa nchini Misri, kilipiga marufuku uvaaji wa niqab kwa walimu wake, uamuzi uliothibitishwa mwaka 2020 na mahakama ya utawala mjini Cairo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.