Pata taarifa kuu

Mafuriko nchini Libya: UN na WHO zatiwa wasiwasi kuhusu hatari za magonjwa

Wiki moja baada ya mafuriko makubwa yaliyosababishwa na kimbunga Daniel huko Derna, mashariki mwa Libya, miili mingi bado imekwama chini ya vifusi. Hali hii inatishia mazingira ya usafi. Wakati huo huo mashirika ya Umoja wa Mataifa yanajaribu kuzuia kuenea kwa magonjwa.

Timu za uokoaji huko Derna, Libya, Jumapili, Septemba 17, 2023.
Timu za uokoaji huko Derna, Libya, Jumapili, Septemba 17, 2023. AP - Yousef Murad
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa unahofia kwamba maji yataambukizwa na kusababisha "mgogoro wa pili mbaya" katika eneo hilo.

Katika taarifa yake, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) umeeleza kuwa timu kutoka mashirika tisa ya Umoja wa Mataifa zilikuwepo kwnye maeneo ya matukio huko Derna na miji mingine ya mashariki mwa Libya kutoa misaada na huduma kwa raia. "Mamlaka za ndani, mashirika ya misaada na timu ya WHO (Shirika la Afya Dunia) wote wana wasiwasi kuhusu hatari ya kuenea kwa magonjwa, kupitia maji machafu na ukosefu wa usafi," kulingana na Umoja wa Mataifa.

Vifaa vya matibabu ya dharura vimesambazwa kwa vituo vya afya na UNICZF​​​​kusaidia watu 15,000 kwa miezi mitatu.

Aidha, mgao wa chakula uligawiwa kwa zaidi ya kaya 5,000 na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na tani 28 za vifaa vya matibabu vilisafirishwa kwa ndege iliyokodishwa na WHO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.