Pata taarifa kuu

CAR : Rais wa zamani Francois Bozize amehukumiwa maisha jela

Kiongozi wa zamani wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni, Francois Bozize, amehukumiwa kifungo cha maisha na kazi ngumu kwa kuongoza uasi na mauaji kwenye taifa hilo.

Kiongozi huyu aliyeingia madarakani mwaka wa 2003 kabla ya kuondolewa baadae, alihukumiwa hapo jana, kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya sheria
Kiongozi huyu aliyeingia madarakani mwaka wa 2003 kabla ya kuondolewa baadae, alihukumiwa hapo jana, kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya sheria Simon Maina/AFP
Matangazo ya kibiashara

Bozize, mwenye umri wa miaka 76 na ambaye alikuwa mafichoni nchini Chad hadi mwezi Machi kabla ya kuhamia nchini Guinea Bissau, anaoongoza muungano wa waasi wanaodai mabadiliko CPC), ambao uliundwa mwezi Desemba mwaka wa 2020.

Kiongozi huyu aliyeingia madarakani mwaka wa 2003 kabla ya kuondolewa baadae, alihukumiwa hapo jana, kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya sheria.

Watoto wawili wakubwa wa Bozize pamoja na watuhumiwa wengine 20 wakiwemo viongozi wa waasi, pia walihukumiwa adhabu kama hiyo bila ya wao kuwepo mahakamani.

Hata hivyo Hukumu hiyo haikuweka wazi ni lini watuhumiwa hao walitenda makosa yenyewe.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yamekuwa yakishuhudiwa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati mojawapo ya mataifa maskini zaidi duniani tangu mwaka wa 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.