Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

DRC: Uganda yatwaa sehemu ya eneo la Busanza, kulingana na mashahidi

Mnamo Septemba 28, Mbunge Juvénal Munubo Mubi aliwasilisha swali akiuliza wakati wa mjadala kwa afisi ya spika wa Bunge la kitaifa. Mbinu ambayo inalenga kupata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje kuhusu shuhuda juu ya madai ya Uganda kunyakua sehemu ya kijiji cha Busanza, kilichoko katika eneo la Rutshuru. Maswali yaliyoulizwa hasa yanahusu uthibitisho wa unyakuzi wa eneo hili pamoja na hatua zinazokusudiwa kuchukuliwa na serikali kuhifadhi uadilifu wa eneo la kitaifa.

Sehemu ya kijiji cha Busanza, kilichoko katika eneo la Rutshuru, ilichukuliwa na Uganda, kulingana na baadhi ya shuhuda.
Sehemu ya kijiji cha Busanza, kilichoko katika eneo la Rutshuru, ilichukuliwa na Uganda, kulingana na baadhi ya shuhuda. (Foto : Roberto Schmidt/AFP)
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Patient Ligodi

Kijiji cha Busanza kwa kiasi kikubwa kiko chini ya udhibiti wa vikosi vya M23, na hivyo kufanya kuwa vigumu kukusanya taarifa za kuaminika. Kwa wakati huu, vyanzo huru havijaweza kuthibitisha au kukanusha madai haya.

Katika hali hii ya mvutano, DRC na Uganda tayari zimekuwa katika mzozo kuhusu uwekaji mipaka ya ardhi, hasa katika eneo la Rutshuru, hasa katika mtaa wa Ishasha, ulioko katika eneo la Binza.

Katika baadhi ya majimbo, mipaka bado haijulikani wazi, na alama za mipaka ziko mbali au hata hazipo, hasa karibu na kijiji cha Kitagoma.

Hali inatofautiana kutoka eneo moja hadi jingine, pamoja na hali ambapo wakazi wa Uganda mara kwa mara hukodi ardhi ya Kongo kulima, hasa, viazi.

Mahusiano kati ya DRC na Uganda yana hali ya sintofahamu, licha ya operesheni za pamoja za kijeshi. Madai haya yanahatarisha kuongezeka kwa hali hii ya kutoaminiana.

Mnamo Juni 2022, kwa mfano, Bunge la kitaifa la DRC lilisitisha uidhinishaji wa mikataba na Uganda, likisema kwamba Kampala ilisaliti Kinshasa kwa kufikia makubaliano na Kigali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.