Pata taarifa kuu

Rais Putin amekutana na mbabe wa kivita wa Libya jijini Moscow

Rais Vladimir Putin wa Urusi amefanya mazungumzo na kiongozi wa kijeshi Mashariki ya Libya Khalifa Haftar jijini Moscow.

Viongozi hao wamejadiliana kuhusu hali ya usalama katika eneo la mashariki ya Libya
Viongozi hao wamejadiliana kuhusu hali ya usalama katika eneo la mashariki ya Libya REUTERS - ESAM OMRAN AL-FETORI
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Jenerali Haftar, vilitegemea pakubwa wapiganaji wa Urusi Wagner, ambao kwa sehemu kubwa bado wangali mashariki mwa Libya.

Msemaji wa Kremlin amesema viongozi hao wamejadiliana kuhusu hali ya nchini Libya na eneo hilo la mashariki.

Vikosi vya Jenerali Haftar vinatawala eneo la mashariki ya Libya, wakati vile vya serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa vikichukua uthibiti wa baadhi ya maeneo ya Magharibi.

Urusi kwa imeonekana kuendelea kutafuta mbinu za kutafuta ushawishi barani Afrika.

Urusi imekuwa ikitafuta ushawishi barani Afrika, Moscow ikionekana kuwa karibu na Jenerali Hifter wa Libya
Urusi imekuwa ikitafuta ushawishi barani Afrika, Moscow ikionekana kuwa karibu na Jenerali Hifter wa Libya AP - Mohammed El-Sheikhy

Huu ulikuwa mkutano wa kwanza kati ya viongozi hao wawili tangu mwaka wa 2019 kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Tripoli.

Mbabe huyo wa kivita wa mashariki ya Libya awali alikuwa amefanya mazungumzo na naibu waziri wa ulinzi wa Moscow Yunus-Bek Yevkurov wakati wa ziara yake.

Libya imekuwa ikikabiliwa na machafuko tangu mwaka wa 2011
Libya imekuwa ikikabiliwa na machafuko tangu mwaka wa 2011 REUTERS - HAZEM AHMED

Yevkurov amekuwa akizuru mashariki ya Libya katika miaka ya hivi karibuni, ziara ya hivi karibuni akiifanya tarehe 17 ya mwezi Septemba.

Wakati wa ziara yake nchini Libya, alikutana na Jenerali Haftar siku chache baada ya kutokea kwa mafuriko mabaya katika mji wa pwani wa Derna, mafuriko yaliosababisha vifo vya maelfu ya watu wakati wengine wakiwa hawajulikani waliko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.