Pata taarifa kuu

Mashirika ya mazingira yawasilisha kesi dhidi ya TotalEnergies

Nairobi – Mashirika manne ya ulinzi wa mazingira yamefungua kesi dhidi ya kampuni ya mafuta ya Ufaransa, TotalEnergies, yakidai inachangia athari za tabia nchi kutokana na mradi wake wa bomba la mafuta kati ya Uganda na Tanzania, mawakili wake wamesema hapo jana.

Katika kesi hiyo, mashirika hayo yanasema, ujenzi wa mradi huo, utasababisha uharibifu mazingira
Katika kesi hiyo, mashirika hayo yanasema, ujenzi wa mradi huo, utasababisha uharibifu mazingira © REUTERS/Sarah Meyssonnier
Matangazo ya kibiashara

Yakiongozwa na Darwin Climax Coalitions na  Sea Shepherd France pamoja na mashirika mengine mawili, yanataka mradi huo kusitishwa.

Mawakili wa  Mashirika hayo, wakiongozwa na  William Bourdon, wamesema kesi hiyo imewasilishwa dhidi ya kampuni hiyo ya TotalEnergies, nchini Ufaransa tangu Septemba 22.

Katika kesi hiyo, mashirika hayo yanasema, ujenzi wa mradi huo, utasababisha uharibifu mazingira, mali na kusababisha maisha ya watu wa nchi hizo mbili.

Licha ya shinikizo hizi, rais Yoweri Museveni ameapa kuwa ni lazima mradi huo uendelee
Licha ya shinikizo hizi, rais Yoweri Museveni ameapa kuwa ni lazima mradi huo uendelee © sahel-intelligence

Mbali na wanaharakati hao, Shirika la kutetea haki za binadamu la  Human Rights Watch linataka pia kusitishwa kwa ujenzi huo, wenye urefu wa Kilomita 1,445 kutoka Hoima nchini Uganda hadi kwenye Bandari ya Tanga nchini Tanzania, wenye thamani ya Dola Bilioni 10.

Licha ya shinikizo hizi, rais Yoweri Museveni ameapa kuwa ni lazima mradi huo uendelee, huku kampuni ya  TotalEnergies ikisema watu zaidi ya Laki Moja, watakaothiriwa na mradi huo, wamelipwa fidia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.