Pata taarifa kuu

CAR: ICC imeondoa mashtaka dhidi ya mwanachama wa zamani wa kundi la waasi

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kibinadamu (ICC) ameondoa mashtaka yote dhidi ya Maxime Mokom, mwanachama wa kundi la waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Maxime Mokom alikuwa anatuhumiwa kwa kuhusika makosa kadhaa ikiwemo mauaji na ubakaji
Maxime Mokom alikuwa anatuhumiwa kwa kuhusika makosa kadhaa ikiwemo mauaji na ubakaji REUTERS - PIROSCHKA VAN DE WOUW
Matangazo ya kibiashara

Mokom amekuwa akizuiliwa na mahakama tangu mwezi Machi Machi mwaka uliopita.

Alituhumiwa kwa makosa kadhaa ikiwemo kutekeleza mashambulio dhidi ya raia, mauaji pamoja na ubakaji wakati akiwa wanachama wa kundi la waasi la anti-balaka nchini Jamhuri ya Afrika ya kati kati ya mwaka wa 2013 na 2014.

Alikuwa amekana mashtaka hayo kwa misingi kuwa alijiunga na kundi hilo kwa nia ya kutafuta amani wala sio vita.

Mokom amekuwa akizuiliwa na mahakama tangu mwezi Machi Machi mwaka uliopita
Mokom amekuwa akizuiliwa na mahakama tangu mwezi Machi Machi mwaka uliopita © Le360 Afrique with AFP

Kwa mujibu wa ICC, machafuko yaliotekelezwa na anti-Balaka na kundi pinzani la Seleka nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, yalisababisha vifo vya maelfu ya raia wakati wengine zaidi ya laki moja wakipoteza makazi yao.

Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo ya ICC Karim Khan alisema baada mahakama hiyo kuangazia ushahidi na suala la upatikanaji wa mashahidi, aliamua hakukuwa na uwezo wa kumhukumu hata kama kesi dhidi yake ingeanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.