Pata taarifa kuu

Guinea: Aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo “Dadis” Camara, ametoroka kutoka Jela

Nchini Guinea, aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Dikteta Moussa “Dadis” Camara, ametoroka kutoka Jela, huku milio ya risasi ikisikika mapema leo jijini Conakry. 

Wakili wa kiongozi huyo wa zamani, Jocamey Haba  amethibitisha kutoroshwa kwa Camara, na kikosi maalum cha makomandoo
Wakili wa kiongozi huyo wa zamani, Jocamey Haba  amethibitisha kutoroshwa kwa Camara, na kikosi maalum cha makomandoo © wikimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Wakili wa kiongozi huyo wa zamani, Jocamey Haba  amethibitisha kutoroshwa kwa Camara, na kikosi maalum cha makomandoo, wanaoripotiwa walikuwa wamejihami kwa silaha. 

Aidha, Haba amesema kuna uwezekano mteja wake,aliondolewa gerezani kwa nguvu huku Waziri wa masuala ya haki Charles Alphonse Wright akisema, Camara ametoroka. 

Kufuatia hatua hiyo, serikali ya kijeshi inayoongoza taifa hilo la Afrika Magharibi imetangaza kufungwa kwa mipaka yote, ikiapa kuwatafuta na kuwachukulia hatua waliohusika na tukio hilo. 

Hili limebainika baada ya mapema leo asubuhi, kuripotiwa makabiliano makali ya risasi katika eneo la Kaloum, makao makuu ya uongozi wa nchi jijini Conakry. 

Mwaka uliopita, Camara alifungwa jela na wenzake baada ya kupatikana na hatia ya kuamuru kuuawa kwa wapinzani katika uwanja wa michezo jijini Conakry na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 150 mwaka 2009. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.