Pata taarifa kuu

Guinea: Msako dhidi ya mwanajeshi wa zamani aliyetoroka jela unaendelea

Nairobi – Nchini Guinea, vyombo vya usalama vinaendelea na msako dhidi ya mwanajeshi na waziri wa zamani kwenye taifa hilo, Claude Pivi, ambaye alitoroka jela mwishoni mwa juma lililopita mjini Conakry.

Wanajeshi wa serikali wa Guinea jijini Conakry
Wanajeshi wa serikali wa Guinea jijini Conakry REUTERS/Saliou Samb
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo tayari kuna malalamiko ya unyanyasaji ulioambata na operesheni za idara za usalama kuhusu msako huo.

Msako huo ulifanyika kwenye mitaa na wilaya za jiji la Conakry mwanzoni mwa juma hili baada ya wanasiasa miongoni mwao Dadis Camara na watu wengine kujaribu kutoroka wakati kesi yao ya tuhuma za mauaji ya waandamanaji ikiwa bado inaendelea.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, askari ambao ni mashahidi wanawataja kuwa ni wa Kikosi Maalumu na walianza upekuzi wao wakizifuata anwani tofauti za Claude Pivi, mmoja huko Coyah,nyingine karibu na Dubréka. Mikoa iliyo karibu na jiji kuu, Conakry.

Mwandishi wa RFI aliyeko Guinea, Sidy Yansané anasema wananchi wameshuhudia kuwa operesheni hizi zinafanyika chini ya unyanyasaji mkubwa, baadhi wakihojiwa kwa ukali na jeuri, na kwamba wengine wamejikuta nyumba zao zikiporwa mali, taarifa ambayo imethibitishwa na mmiliki wa baa maarufu mjini Conakry Mamadou Souaré Diop.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.