Pata taarifa kuu
RUSHWA-HAKI

Paris yapanga kurejesha euro milioni sita kwa Equatorial Guinea

Kwa mara ya kwanza, bajeti ya serikali ya Ufaransa, kwa mwaka wa 2024, inapanga kurudisha euro milioni sita kwa Equatorial Guinea katika muktadha wa mali iliyopatikana kwa njia isiyo halali ambayo ilitumiwa kukuza ufisadi.

Teodorin Obiang, makamu wa rais wa Equatorial Guinea, Mei 2019.
Teodorin Obiang, makamu wa rais wa Equatorial Guinea, Mei 2019. Michele Spatari / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kiasi hiki cha euro milioni sita kinalingana na mali iliyokamatwa na mahakama ya Ufaransa, ambayo ni magari na vitu vya anasa vilivyokuwa vya Teodorin Obiang, makamu wa rais wa Equatorial Guinea na mtoto wa rais. Pia miongoni mwa mali zilizopatikana kwa njia haramu ni jumba la kifahari huko Paris lenye thamani ya zaidi ya euro milioni 100, ambalo leo linakaliwa na ubalozi wa Equatorial Guinea.

Kwa jumla, euro milioni 150

Kwa jumla, kiasi ya mali iliyochukuliwa inakadiriwa kuwa euro milioni 150. Transparency International, shirika lisilo la kiserikali la kimataifa linalopambana dhidi ya rushwa na hongo kote duniani linakaribisha mradi huu wa kurejesha fedha na kutoa wito wa ufuatiliaji makini wa matumizi yatakayofanywa kwa pesa hizi.

"Katika nchi kama Equatorial Guinea ambako kuna serikali imeshikiliwa na kundi la watu, utawala ambao umekuwepo kwa zaidi ya miaka 40, na ufisadi ambao umekithiri, ni hakika kwamba kama pesa hizi zitarejeshwa -  kutoka Hazina ya Ufaransa kwenda Hazina ya Equatorial Guinea – hatutaona miradi mingi ya manufaa ya jumla ikifadhiliwa na fedha hizi zilizorejeshwa,” anasisitiza Sara Brimbeuf, mtaalamu wa bidhaa zilizopatikana kwa njia isiyohalali katika shirika la Transparency International.

"Uwazi"

Kabla ya kuongeza kuwa “ dira ya utaratibu wowote wa urejeshaji fedha ni uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa mashirika ya kiraia, ya Ufaransa lakini hasa mashirika ya kiraia ya Equatorial Guinea. Hivyo, ili kuweza kuhakikisha kuwa bidhaa zinarudishwa karibu iwezekanavyo na wananchi kwa ajili ya miradi yenye manufaa kwao, inayokidhi mahitaji yao, ni muhimu, katika lengo hili la haki, kuhakikisha kwamba fedha hizo zinaishia pale ambapo zilipaswa kwenda, yaani kwa manufaa ya wananchi na isirudi kwenye mifuko ya viongozi mafisadi kwa sababu hiyo itamaanisha kuwa taratibu zote hizi, miaka yote ya taratibu za kisheria, hatimaye hazikuchangia chochote.”

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.