Pata taarifa kuu

Jeshi laagiza kufunguliwa mashitaka kwa Condé

Utawala wa kijeshi nchini Guinea umeagiza kufunguliwa mashtaka mapya dhidi ya rais wa zamani Alpha Condé, ambaye ulimpindua madarakani kupitia mapinduzi mwaka 2021, kwa madai ya vitendo vya "uhaini", imesema barua kutoka kwa waziri wa Sheria alioituma kwa Mwanasheria Mkuu wa Conakry leo Jumanne.

Mnamo 2010, Alpha Condé alikua rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Guinea baada ya miongo kadhaa ya tawala za kimabavu au kidikteta.
Mnamo 2010, Alpha Condé alikua rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Guinea baada ya miongo kadhaa ya tawala za kimabavu au kidikteta. © Carol Valade/RFI
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa zamani kuanzia mwaka 2010 hadi 2021, akiwa uhamishoni nchini Uturuki tangu aondolewe madarakani, anashitakiwa kwa madai ya vitendo vya "ufisadi", pamoja na "mauaji, vitendo vya utesaji, utekaji nyara na ubakaji".

"Mumeagizwa (...) kuanzisha kesi za kisheria kwa madai ya vitendo vya uhaini, njama ya jinai na kushiriki katika umiliki haramu wa silaha dhidi ya Profesa Alpha Condé, Rais wa zamani wa Jamhuri", ameandika Waziri wa Sheria Alphonse Charles Wright. "Inafahamishwa kwa Waziri wa Sheria (...) kwamba Alpha Condé, kwa kushirikiana na Bw. Fodé Moussa Mara", mwanablogu maarufu mfuasi wa Bw. Condé, "ametumia njia kupata silaha, risasi na vifaa vinavyohusiana,” Bw. Wright amesema katika barua hiyo ya umma iliyoandikwa siku ya Jumatatu. Hakutoa taarifa zaidi kuhusu asili na wingi wa silaha hizi.

Mnamo mwaka wa 2010, Alpha Condé alikua rais wa kwanza wa Guinea kuchaguliwa kidemokrasia baada ya miongo kadhaa ya tawala za kimabavu au za kidikteta, lakini nia yake ya kusalia madarakani ili kugombea muhula wa tatu iliibua maandamano makubwa, yaliyokandamizwa vikali, hadi kuanguka kwake.

Baada ya mapinduzi ya mwaka wa 2021, Kanali Mamady Doumbouya alitawazwa kuwa rais na chini ya shinikizo la kimataifa alijitolea kukabidhi mamlaka kwa raia waliochaguliwa ndani ya miaka miwili kuanzia Januari 2023. Aliahidi kujenga upya nchi iliyodhoofishwa na migawanyiko na rushwa inayoonekana kuwa mbaya. Serikali yake imeanzisha idadi kubwa ya mashtaka dhidi ya watu walio karibu na rais wa zamani Condé.

Mapinduzi ya Septemba 5, 2021 ni mojawapo ya matukio kadhaa na majaribio ya mapinduzi ambayo yametikisa Afrika Magharibi tangu jeshi kuchukua mamlaka nchini Mali mnamo Agosti 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.