Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Bunge lapitisha muswada unaopendekeza kufungwa kwa ubalozi wa Israeli

Wabunge nchini Afrika Kusini, wamepiga kura inayopendekeza kufungwa kwa ubalozi wa Israeli mjini Pretoria pamoja na kusitishwa kwa uhusiano wowote wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Rampahosa aliongoza kikao cha nchi za Brics siku ya Jummane kwa njia ya mtandao ambapo walijadili kuhusu hali ya Gaza
Rampahosa aliongoza kikao cha nchi za Brics siku ya Jummane kwa njia ya mtandao ambapo walijadili kuhusu hali ya Gaza AP
Matangazo ya kibiashara

Chama tawala cha ANC ambacho kina uwakilishwaji mkubwa kwenye bunge, kimekuwa kikiituhumu Israeli kuhsiana na oparesheni zake katika ukanda wa Gaza na kimeunga mkono muswada huo kwenye bunge.

Wabunge wamesema wamepitisha muswada huo unaoruhusu kufungwa kwa ubalozi wa Israeli na kusitishwa kwa uhusiano wa kidplomasia hadi pale Israeli itakapokubali kusitishwa kwa mapigano na kuruhusu mazunguzmo yenye tija.

Muswada huo uliuungwa mkono na wabunge 248 dhidi ya 91.

Jeshi la Israeli limekuwa likitekeleza oparesheni katika ukanda wa Gaza kuwasaka wapiganaji wa Hamas
Jeshi la Israeli limekuwa likitekeleza oparesheni katika ukanda wa Gaza kuwasaka wapiganaji wa Hamas © IDF

Kuelekea upigaji kura kuhusiana na muswada huo, Israeli ilimuita nyumbani balozi wake kwa majadiliano, hatua ambayo ilisema imetokana na matamshi ya taifa hilo la Afrika.

Hivi majuzi, rais Cyril Ramaphosa alisema nchi ya Israeli inafaa kuwajibishwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC kutokana na kile alichosema ni ukiukaji wa haki za binadamu. Afrika Kusini pia ilimwagiza balozi wake nchini Israeli kurejea nyumbani.

Ramaphosa aliongoza kikao cha Bricks ambacho kilijadili hali ya Gaza wiki hii
Ramaphosa aliongoza kikao cha Bricks ambacho kilijadili hali ya Gaza wiki hii AP - Themba Hadebe

Rampahosa aliongoza kikao cha nchi za Brics siku ya Jummane kwa njia ya mtandao ambapo walijadili kuhusu hali ya Gaza.

Israel imetetea oparesheni zake katika ukanda wa Gaza kwa misingi kuwa inajilinda na inalenga kuwaondoa wapiganaji wa Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.