Pata taarifa kuu

Sierra Leone: Mamlaka imelegeza makataa ya watu kutembea nje

Sierra Leone imeondoa makataa ya watu kutembea nje nchi nzima iliyokuwa imetangazwa siku ya Jumapili baada ya watu wenye silaha kutekeleza shambulio kwenye kambi ya jeshi na kuwatorosha wafungwa katika baadhi ya magereza katika mji mkuu wa Freetown.

Rais Bio aliwahakikishia raia wa nchi yake kuwa hali ya utulivu imerejeshwa licha ya kilichotokea
Rais Bio aliwahakikishia raia wa nchi yake kuwa hali ya utulivu imerejeshwa licha ya kilichotokea © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa makataa ya watu kutembea nje usiku yanatarajiwa kuaanza saa tatu usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi kila siku hadi tangazo lengine litakapotolewa.

Katika taarifa yake kwa taifa siku ya Jumapili, Rais Julius Maada Bio alisema kuwa sehemu kubwa ya watu waliohusika katika machafuko hayo ya Jumapili wamekamatwa na watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Aidha rais Bio aliwahakikishia raia wa nchi yake kuwa hali ya utulivu imerejeshwa licha ya kilichotokea.

Mkuu wa nchi pia alitaja kilichotokea kama shambulio dhidi ya demokrasia lakini hakuwataja watu waliohusika wala kuzungumzia jaribio hilo la mapinduzi.

Watu hao wenye silaha wamesemekana kuwaachia wafungwa wakati wa uvamizi huo pamoja na kuwateka wengine.

Rais Bio alichaguliwa kwa muhula mwengine mwezi Juni lakini mwezi Agosti, baadhi ya maofisa wa jeshi walikamatwa kwa tuhuma za kupanga mapinduzi dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.