Pata taarifa kuu

Uganda kupokea mkopo kutoka kwa benki ya China

Nchi ya Uganda inajiandaa kukopa dolla millioni 150, kutoka kwa benki ya China ya (Exim), kufanikisha miradi yake baada ya benki ya dunia kusitisha misaada yake kwa nchi hiyo kutokana  na sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.

Rais Museveni alitia saini sheria inayopinga mapenzi ya jinsia moja
Rais Museveni alitia saini sheria inayopinga mapenzi ya jinsia moja © SERIKALI YA UGANDA
Matangazo ya kibiashara

Uganda inakopa pesa hizo kwa benki ya EXIM, ili kuimarisha miundo mbinu yake ya mitandao, wizara ya fedha nchini humo imetangaza, wakati huu Uganda ikiendelea kutegemea mikopo kujiendeleza.

Wizara ya feha nchini humo sasa ikilitaka bunge, kuidhinisha serikali kuomba mkopo huo kutoka China.

Benki ya Dunia ambayo ndiyo ilikuwa  mshirika mkuu wa Uganda na pia mkopeshaji wake, ilisitisha uhusiano na taifa hilo la Afrika mashariki baada ya rais Yoweri Museveni, kuidhinisha sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ikiwemo kuwaadhibu na hukumu ya kifo, sheria ambao pia imekashifiwa na mataifa kadhaa ikiwemo Marekani na Umoja wa Ulaya.

Licha ya hayo rais Muveseni amesiitiza kwamba serikali yake haitalegeza kamba katika kutekeleza sheria hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.