Pata taarifa kuu

Marekani: Makundi yanayopigana DRC, yamekubali kusitisha mapigano kwa saa 72

NAIROBI – Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kumeripotiwa usitishwaji wa mapigano wa saa 72 kati ya wanajeshi wa serikali FARDC na waasi wa M23 wanaodawa kuungwa mkono na Rwanda.

Wapiganaji wa M23, mashariki mwa DRC
Wapiganaji wa M23, mashariki mwa DRC AP - Moses Sawasawa
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya Marekani kupitia msemaji wa Baraza la Usalama, Adrienne Watson,  imetangaza hatua hii na kusema itatumia mbinu zake za Kiintelijensia na watalaam wake kufuatilia utekelezwaji wa mkataba huo wa kusitisha mapigano.

Kusitishwa kwa mapigano hayo kunawezesha kuondoka kwa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambavyo vimekuwa vikidhibiti maeneo ya Mushaki na viunga vyake.

Hata hivyo, serikali ya DRC na Rwanda, hazijazungumzia tangazo hilo la Marekani ambayo imekuwa ikitoa wito kwa utulivu kati ya makundi ya waasi yanayodaiwa kuungwa mkono na nchi hizo jirani na kusababisha hali mbaya ya kibindamu mpakani.

Mwezi Novemva mwaka uliopita, kulikuwa na mkataba mwingine wa usitishwaji wa mapigano, lakini waasi wa M23 wakadaiwa kuuvunja.

DRC imeendelea kuishtumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 madai ambayo Kigali imeendelea kupinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.