Pata taarifa kuu

Gerco van Deventer achiliwa baada ya miaka sita ya kushikiliwa mateka

Gerco van Deventer alitekwa nyara nchini Libya mnamo Novemba 2017 kisha kuuzwa kwa Kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (JNIM na kuhamishiwa nchini Mali ambako alishiriki sehemu ya utumwa wake na mateka Mfaransa Olivier Dubois. Aliachiliwa Jumamosi Desemba 16 na kukabidhiwa kwa mamlaka ya Algeria kwenye mpaka na Mali, kulingana na wakfu wa Afrika Kusini Gift of the Givers, ambao umekuwa mpatanishi tangu mwaka 2018.

Gerco van Deventer. Picha isiyo na tarehe iliyopigwa na familia yake.
Gerco van Deventer. Picha isiyo na tarehe iliyopigwa na familia yake. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Mateka wa Afrika Kusini Gerco van Deventer ataweza kucheherekea Krismasi na familia yake. Aliachiliwa Jumamosi Desemba 16 na kukabidhiwa kwa mamlaka ya Algeria kwenye mpaka na Mali, kwa mujibu wa wakfu wa Gift of the Givers wa Afrika Kusini ambao umekuwa mpatanishi tangu 2018. Kulingana na wakfu huo, hakuna fidia iliyolipwa, anaripoti mwandishi wetu. Johannesburg, Romain Chanson. Familia haikuweza kumudu kulipa fidia ya awali ya dola milioni tatu, ambayo ilipunguzwa hadi dola 500,000 na ambayo ilishuka hadi sifuri.

Taasisi hiyo inasema ilipokea simu kutoka kwa Mmauritania mmoja mnamo Desemba 5 ambaye alieleza kuwa alikuwa akifanya kazi ya kumwachilia Gerco van Deventer. Hatimaye ni kupitia Algeria ambapo Mwafrika Kusini aliachiliwa na kupelekwa hospitali kufanyiwa uchunguzi wa afya. Gerco van Deventer alipigwa risasi kwenye mkono wake wa kushoto alipokuwa kizuizini.

Miaka sita kizuizini

Kuachiliwa kwa Gerco van Deventer kunamaliza zaidi ya miaka sita ya kizuizini. Mhudumu huyu wa afya wa Afrika Kusini alitekwa nyara mnamo Novemba 3, 2017 kusini mwa Libya kabla ya kuuzwa kwa Kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (JNIM), lenye uhusiano na al-Qaeda, na kuhamishiwa kaskazini mwa Mali.

Mwanahabari Mfaransa Olivier Dubois, aliyeachiliwa mnamo Machi 20, 2023, alibaini kwamba alikaa kifungoni kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu akiwa na Gerco van Deventer katika jangwa la Mali. Baba huyu wa watoto watatu hatimaye ataweza kuungana na familia yake, mkewe Shereen ambaye aliendelea kutangaza kesi yake, wakati mwingine kwa kutojali.

Alipowasiliana na RFI, mke wa Gerco van Deventer, Shereen, amesema bado anasubiri uthibitisho madhubuti wa kuachiliwa kwake. Kwa upande wa Afrika Kusini, mamlaka bado haijachukua hatua licha ya kupata taarifa kutoka  kwetu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.