Pata taarifa kuu

UN yakosoa rekodi ya uhuru wa vyombo vya Habari nchini Guinea

Umoja wa Mataifa unasema, unaguswa na ongezeko la uminywaji wa uhuru wa vyombo vya Habari nchini Guinea, taifa la Afrika Magharibi, linaloongozwa na jeshi.

Kiongozi wa kijeshi nchini Guinea Mamady Doumbouya
Kiongozi wa kijeshi nchini Guinea Mamady Doumbouya AP
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwezi Mei, uongozi wa kijeshi umeweka vikwazo vingi kwa vyombo vya Habari vya kibinafsi ambavyo vimefungiwa na wanahabari wakikamatwa na kuzuiwa jela.

Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Volker Turk ameutaka uongozi wa kijeshi kubadilisha haraka hatua ya kuminya uhuru wa vyombi vya Habari.

Aidha, imebainika kuwa vifaa vya kurusha matangazo, vimeharibiwa na uongozi wa kijeshi huku wanahabari wakitishiwa na hata kupigwa wakati wakitekeleza majukumu yao.

Mitandao ya kijamii imezuiwa na kuwaacha wananchi kutokuwa na uwezo wa kufungumia tovuti mbalimbali za kupata habari kama ilivyokuwa miaka ya awali.

Tangu tarehe 24 mwezi Novemba mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, WhatsApp na TikTok imezuiwa nchini humo, huku huduma ya mtandao wa internet ukitatizwa kwa miezi saba sasa na uongozi wa kijeshi ambao umekuwa madarakani tangu Septemba 2021.

Guinea inaorodheshwa katika nafasi ya 85 kati ya nchi 180 na Shirika la Kimataifa la Reporters Without Borders kuhusu uhuru wa vyombo vya Habari duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.