Pata taarifa kuu

Mpiga picha Peter Magubane, mwandishi wa historia ya ubaguzi wa rangi afariki dunia

Mwanahabari na mpiga picha Mweusi wa Afrika Kusini Peter Magubane, ambaye kwa miongo kadhaa aliandika ghasia za utawala wa kibaguzi, ikiwa ni pamoja na uasi wa wanafunzi wa Soweto mwaka 1976, amefariki dunia siku ya Jumatatu akiwa na umri wa miaka 91, familia yake imetangaza.

Mpiga picha Peter Magubane wakati wa toleo la 26 la Mwaka za Kituo cha International Center of Photography Infinity Awards katika Pier Sixty, Chelsea Piers mnamo Mei 10, 2010 huko New York.
Mpiga picha Peter Magubane wakati wa toleo la 26 la Mwaka za Kituo cha International Center of Photography Infinity Awards katika Pier Sixty, Chelsea Piers mnamo Mei 10, 2010 huko New York. Getty Images via AFP - STEPHEN LOVEKIN
Matangazo ya kibiashara

Wakati mwanaharakati mkuu wa kupinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela alipoachiliwa huru mwaka 1990, Magubane alikua mpiga picha wake rasmi hadi kuchaguliwa kwake miaka minne baadaye kama rais wa kwanza mweusi, wakati wa ujio wa demokrasia nchini humo. "Almefariki leo kwa amani, akiwa amezungukwa na familia yake," limetangaza baraza la uwakilishi la vyombo vya habari vya Afrika Kusini, SANEF.

Alikuwa "mpiga picha makini, mwenye bidii katika kazi", amesema binti yake Fikile kwenye idhaa ya umma ya SABC. "Alikuwa na shauku, kazi yake ilikuwa kipaumbele chake cha juu." "Afrika Kusini imempoteza mpigania uhuru, msimuliaji hadithi na mpiga picha," Waziri wa Utamaduni Zizi Kodwa aliandika kwenye kurasa wake wa Twitter. Peter Magubane bila woga aliandika dhuluma za ubaguzi wa rangi.

Mojawapo ya picha zake maarufu, iliyotoka mwaka wa 1956, inaonyesha msichana mdogo mweupe kwenye benchi iliyoandikwa "Wazungu pekee", yaya wake mweusi akiwa ameketi upande wa pili wa benchi katika kitongoji cha Johannesburg. Baada ya kuanza kama dereva wa Gazeti maarufu la Drum, linalojishughulisha na utamaduni wa watu weusi wa mijini, alihamia kwenye maabara ya picha kabla ya kujiweka nyuma ya lenzi. Aliandika maisha ya kila siku na matukio kadhaa muhimu katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Alikamatwa mwaka 1969 wakati akipiga picha waandamanaji mbele ya gereza alimokuwa mwanaharakati Winnie Mandela, alikaa siku 586 katika kifungo cha upweke gerezani na alihukumiwa baada ya kuachiliwa kusitisha shughuli zote za upigaji picha kwa miaka mitano. Mnamo 1971, alikamatwa tena na kufungwa kwa miezi mingi kwa kutotii amri hii.

Akiwa amenyanyaswa na polisi, ambao aliwazuia kadiri iwezekanavyo, aliangazia kwa mapana maasi ya wanafunzi huko Soweto mnamo 1976, ambayo alichukua picha kadhaa za kushangaza zaidi ambazo zilimfanya ajulikane ulimwenguni kote. Peter Magubane amechapisha takriban vitabu kumi na tano, ambavyo vingi vilidhibitiwa chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi, utawala wa ubaguzi ambao ulitawala nchini Afrika Kusini kuanzia mwaka 1948 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.