Pata taarifa kuu

Sierra Leone: Rais wa zamani Koroma ashtakiwa kufuatia 'jaribio la mapinduzi'

Rais wa zamani wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma, ambaye aliongoza nchi hiyo kutoka 2007 hadi 2018, ameshtakiwa siku ya Jumatano kwa jukumu lake katika matukio ya Novemba 26, yaliyoelezwa na serikali kama "jaribio la mapinduzi".

Ernest Bai Koroma hadi wakati huo alikuwa "mtuhumiwa" kwa matukio ya Novemba 26 na alihojiwa mara kadhaa na polisi.
Ernest Bai Koroma hadi wakati huo alikuwa "mtuhumiwa" kwa matukio ya Novemba 26 na alihojiwa mara kadhaa na polisi. Reuters/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

"Rais huyo wa zamani anashtakiwa kwa makosa manne, ikiwa ni pamoja na uhaini na kuficha uhaini," imesema taarifa ya serikali iliyotiwa saini na Waziri wa Habari Chernor A. Bah. Mapema Novemba 26, watu waliojihami kwa bunduki walishambulia ghala la kijeshi, kambi nyingine mbili, magereza mawili na vituo viwili vya polisi, wakikabiliana na vikosi vya usalama.

Mapigano hayo yalisababisha vifo vya watu 21, askari 14, askari polisi mmoja, askari magereza, afisa wa usalama, mwanamke mmoja na washambuliaji watatu, kwa mujibu wa Waziri wa Habari. Takriban watu themanini walikamatwa kuhusiana na matukio haya, hasa askari, kulingana na mamlaka.

Bw. Koroma hadi wakati huo alikuwa "mtuhumiwa" kwa matukio ya Novemba 26 na alihojiwa mara kadhaa na polisi. Tangu Desemba 9, amewekwa chini ya utawala unaofanana na kifungo cha nyumbani. "Rais wa zamani anarejea nyumbani," mmoja wa mawakili wake, Ady Macaulay, ameliambia shirika la habari la AFP. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 17, ameongeza.

Usalama mkubwa uliwekwa karibu na mahakama ya Freetown ambako Bw. Koroma alikuwa akisikilizwa. Siku ya Jumanne, mahakama ya Sierra Leone iliwafungulia mashtaka watuhumiwa kumi na wawili wa "jaribio la mapinduzi", akiwemo Amadu Koita, mwanajeshi wa zamani na mlinzi wa Bw. Koroma, alifuatiliwa sana kwenye mitandao ya kijamii ambapo alikuwa akiikosoa serikali ya rais Julius Maada Bio, kulingana na polisi.

ECOWAS

Mnamo tarehe 23 Desemba, wajumbe wa ngazi ya juu kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) wakiongozwa na marais wa Senegal na Ghana walikutana na Bw. Koroma na rais wa sasa Julius Maada Bio.

Kulingana na Ishmael Sheriff, mshauri wa Bw. Koroma, rais huyo wa zamani yuko kwenye majadiliano ya kuhamishwa nchini Nigeria, nchi yenye nguvu katika eneo hilo ambalo kwa sasa linashikilia urais wa ECOWAS, ameliambia shirika AFP kabla ya kutangazwa kwa mashtaka.

Wakati wa mkutano wa hivi punde wa jumuiya hiyo, wakuu wa nchi wa kanda hiyo waliitaka tume "kuwezesha kutumwa kwa ujumbe wa usalama wa ECOWAS nchini Sierra Leone ili kusaidia kuleta utulivu nchini humo."

Kulingana na mkuu wa diplomasia ya Sierra Leone, "ECOWAS imejenga bohari ya vifaa na ugavi ya Ecomog (kikosi cha amani cha Afrika Magharibi) huko Lungi", mji ulio kaskazini mwa Freetown, "ambayo imekamilika na itaanza kutumika mwezi wa Januari. Kikosi cha kuleta utulivu "sio kikosi cha kuingilia kijeshi", "ni ujumbe wa kulinda amani", amesisitiza Bw. Kabba.

Sheria ya kutotoka nje iliyowekwa tangu matukio ya Novemba 26 iliondolewa mnamo Desemba 20. Kanda ya Afrika Magharibi inakumbwa tangu 2020 naongezeko la mapinduzi ya kijeshi. Mali, Burkina Faso, Niger na Guinea, ni nchi ambazo zimekumbwa na majaribio kadhaa ya mapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.