Pata taarifa kuu

Mkuu wa RSF Hamdan Daglo amezuru Kenya

Nairobi – Kiongozi wa kikosi cha wanamgambo nchini Sudan cha RSF Mohamed Hamdan Daglo jana alikutana na kuzungumza na rais wa Kenya William Ruto, katika mwendelezo wa jitihada za kidiplomasia za kikanda kujaribu kutafuta mwafaka wa usitishwaji wa vita kati ya kikosi chake na wanajeshi wa taifa.

Kabla ya kuzuru Kenya, Daglo, alifanya ziara kama hicyo nchini Djibouti, Ethiopia na Uganda alikokutana na viongozi wa nchi hizo za kikanda
Kabla ya kuzuru Kenya, Daglo, alifanya ziara kama hicyo nchini Djibouti, Ethiopia na Uganda alikokutana na viongozi wa nchi hizo za kikanda © capture d'écran/lemonde.fr/afrique
Matangazo ya kibiashara

Rais Ruto alionekana kwenye picha akimkaribisha Daglo, kwenye Ikulu ya Nairobi ambapo walikuwa na kikao cha siri.

Baada ya kikao hicho kiongozi huyo wa RSF kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, amesema alimwelezea Ruto chanzo cha vita, suluhu ya mzozo unaoendelea na namna ya kuwasaidia watu walioathiriwa.

Kabla ya kuzuru Kenya, Daglo, alifanya ziara kama hicyo nchini Djibouti, Ethiopia na Uganda alikokutana na viongozi wa nchi hizo za kikanda.

Mkuu wa RSF nchini Sudan Mohamed Hamdan Dagalo alikutana na rais wa Kenya, William Ruto
Mkuu wa RSF nchini Sudan Mohamed Hamdan Dagalo alikutana na rais wa Kenya, William Ruto © William Ruto

Ziara hii imekuja kuelekea mkutano muhimu wa kikanda, unaotarajiwa kufanyika nchini Djibouti chini ya muungano wa nchi za IGAD, kujaribu kumpatanisha Daglo, na kiongozi wa kijeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

Mwezi Novemba mwaka uliopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilitoa ripoti kuonesha namna hali inavyoendelea kuwa mbaya nchini Sudan, ambapo tangu mwezi Aprili mwaka ulipita, watu zaidi ya Elfu 12 wamepoteza maisha na kuwaacha wengine zaidi ya Milioni 1.5 wakiimbia nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.