Pata taarifa kuu
SHERIA-HAKI

Oscar Pistorius aachiliwa kwa msamaha

Bingwa wa zamani wa Olimpiki ya Walemavu nchini Afrika Kusini Oscar Pistorius ameachiliwa kutoka gerezani siku ya Ijumaa, kwa siri, na "sasa yuko nyumbani", kwa msamaha, karibu miaka kumi na moja baada ya mauaji ya mpenzi wake, Reeva Steenkamp.

Mwaka mmoja mapema, Oscar Pistorius aliingia kwenye historia kwa kupanga safu na watu wazima katika mita 400 za Michezo ya Olimpiki ya London, ya kwanza kwa mtu aliyekatwa miguu yote miwili.
Mwaka mmoja mapema, Oscar Pistorius aliingia kwenye historia kwa kupanga safu na watu wazima katika mita 400 za Michezo ya Olimpiki ya London, ya kwanza kwa mtu aliyekatwa miguu yote miwili. © Reuters/David Gray
Matangazo ya kibiashara

Mwanariadha huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 37, aliyekatwa miguu yote miwili, aliyepatikana na hatia ya mauaji katika kesi iliyosisimua dunia na ambaye alitumikia zaidi ya nusu ya kifungo chake, aliondoka katika gereza la Atteridgeville mapema asubuhi, katika viunga vya mji mkuu Pretoria. "Amekubaliwa kwa mfumo wa marekebisho ya jamii na sasa yuko nyumbani," mamlaka ya magereza imesema katika taarifa, ikithibitisha kuwa kuachiliwa kwake kwa msamaha sasa kunafaa.

Wala muda wala maelezo ya vifaa hayakuwa yamewasilishwa kabla na mamlaka ambayo ilitaja sababu za "usalama". Bingwa huyo mara sita wa Olimpiki ya walemavu amepigwa marufuku kuzungumza na vyombo vya habari.

Katika taarifa iliyoandikwa na shirika la habari la AFP dakika chache kabla ya kuachiliwa kwa Pistorius, mama wa mwathiriwa alitangaza kuwa ndugu wa Reeva Steenkamp "wamehukumiwa kifungo cha maisha". "Sisi, ambao bado tuko hapa, tumehukumiwa kifungo cha maisha," amesema June Steenkamp. Akiuliza kama "haki imetendewa kwa Reeva" na kama "Oscar ametumikia muda wa kutosha", ameeleza kuwa "hakuna haki kamwe kwa kiwango ambacho mpendwa wako hatarudi tena."

Familia ya Steenkamp haikupinga rasmi kuachiliwa kwa masharti kwa bingwa huyo wa zamani. Lakini June Steenkamp alisema bado haamini "toleo la ukweli la Oscar" na alishawishika kuwa Oscar "hakujirekebisha" akiwa kizuizini.

Udhibiti wa hasira

Usiku wa Februari 13 hadi 14, 2013, Oscar Pistorius alimuua mwanamitindo Reeva Steenkamp, ​​29, kwa kufyatua risasi nne kupitia mlango wa bafuni wa chumba chake cha kulala, katika nyumba yake iliyokuwa na ulinzi mkali mjini Pretoria. Mwaka mmoja mapema, mwanariadha huyo aliingia kwenye hadithi kwa kupanga safu na watu wazima katika mita 400 za Michezo ya Olimpiki ya London, ya kwanza kwa mtu aliyekatwa miguu yote miwili.

Alipokamatwa mapema asubuhi ya Siku ya Wapendanao 2013, Pistorius alikanusha kuwa alifyatua risasi akiwa na hasira, akidai kuwa aliamini kuwepo kwa mwizi. Toleo ambalo alidumisha katika sakata ya kisheria ambayo iliweka vyombo vya habari katika mashaka kwa miaka minne iliyofuata. Mwishoni mwa kesi yake ya kwanza iliyofunguliwa mwaka wa 2014 na kutangazwa moja kwa moja kwenye runinga, mkimbiaji huyo aliyepewa jina la utani la "Blade runner", ikimaanisha bandia zake za kaboni, alipokea kifungo cha miaka mitano jela kwa kuua bila kukusudia.

Sheria ya Afrika Kusini inasema kwamba mfungwa anastahili kurekebishwa hukumu mara baada ya nusu ya kifungo chake kuisha. Mwishoni mwa mwezi wa Novemba, uongozi wa magereza ulitangaza kuachiliwa mapema kwa Oscar Pistorius.

Kama sehemu ya kuwekwa kwake kwa msamaha hadi mwisho wa kifungo chake mnamo 2029, Oscar Pistorius lazima afuate tiba ya kudhibiti hasira na mpango wa unyanyasaji dhidi ya wanawake. Haruhusiwi kunywa pombe. Ni lazima pia atekeleze huduma za jamii, lakini lazima awepo katika nyumba maalum katika kitongoji cha Pretoria katika baadhi ya nyakati za siku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.