Pata taarifa kuu

Sudan yamrejesha nyumbani balozi wake jijini Nairobi

Nairobi – Sudan imemrudisha nyumbani balozi wake kutoka nchini Kenya, baada ya rais William Ruto kukutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa kikosi cha wanamgambo cha RSF Mohamed Hamdan Daglo wiki hii.

Mkuu wa RSF nchini Sudan Mohamed Hamdan Dagalo amekutana na rais wa Kenya, William Ruto
Mkuu wa RSF nchini Sudan Mohamed Hamdan Dagalo amekutana na rais wa Kenya, William Ruto © William Ruto
Matangazo ya kibiashara

Kaimu Waziri wa Mambo ya nje wa Sudan, Ali al-Sadiq amerejeshwa jijiji Khartoum kwa mashauriano zaidi, kufuatia kitendo cha Kenya kumpa makaribisho rasmi Daglo, alipozuru jijini Nairobi.

Wachambuzi wa mambo wanasema hatua hii haishangazi kwa sababu, serikali ya Kenya imeonekana kuwa karibu na Daglo kwenye harakati za kujaribu kutatua mzozo unaoendelea nchini Sudan.

Hatua hii inakuja baada ya kiongozi wa kijeshi Janerali Abdel Fattah al-Burhan, kuonya viongozi wa mataifa ya Afrika kuendelea kumpokea Daglo akimwelezea kama muuaji wa raia wa Sudan.

Mbali na Kenya, Dagalo ambaye kwa siku ya Alhamisi alizuru jijini Pretoria na kukutana na rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa , alitembelea pia Uganda, Ethiopia na Djibouti.

Kiongozi huyo wa RSF pia alizuru Afrika Kusini ambapo alikutana na rais Cyril Ramaphosa
Kiongozi huyo wa RSF pia alizuru Afrika Kusini ambapo alikutana na rais Cyril Ramaphosa via REUTERS - GOVERNMENT COMMUNICATION AND INF

Jumuiya ya nchi za IGAD imepanga kukutanisha pande zinazozona nchini Sudan kwa ajili ya mazungumzo katika siku zijazo nchini Djibouti, ili kumaliza vita ambavyo vilianza mwezi Aprili mwaka uliopita, na mpaka sasa vimesababisha vifo vya watu zaidi ya Elfu 12.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.