Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Uchunguzi wa mauaji manne chini ya ubaguzi wa rangi wafunguliwa tena

Mahakama ya Afrika Kusini imetangaza siku ya Ijumaa kuwa inafungua upya uchunguzi wa mauaji ya wanaharakati wanne waliokuwa wakipambana dhidi ya ubaguzi wa rangi, yanayojulikana kama "mauaji ya Cradock", miongoni mwa uhalifu unaojulikana zaidi na mbaya zaidi wa ubaguzi wa rangi, ambao haujawahi kushuhughulikiwa.

Serikali ya Afrika Kusini inataka kurejesha imani katika mfumo wa mahakama.
Serikali ya Afrika Kusini inataka kurejesha imani katika mfumo wa mahakama. © REUTERS - SUMAYA HISHAM
Matangazo ya kibiashara

"Waziri wa Sheria amefuata pendekezo kutoka kwa Mamlaka ya Kitaifa ya Mashtaka ya Afrika Kusini (...) kuteua jaji kufungua upya na kuongoza uchunguzi wa vifo hivyo," wizara yake imesema katika taarifa.

Tukio hilo lililozua taharuki nchini, lilianza mwaka 1985. Baadae, usiku mmoja wa majira ya baridi kali kusini mwa nchi, wanaharakati wanne Matthew Goniwe, Fort Calata, Sparrow Mkonto na Sicelo Mhlauli, walitoka kwenye mkutano na kuchukua barabara kurejea nyumbani, mji mdogo wa Cradock (kusini).

Hawakufika wanakoenda. Miili yao, iliyochomwa vibaya na kukatwa na visu, iligunduliwa baadaye, katika sehemu mbili tofauti. Wakati huo, vikosi vya usalama vya serikali ya Wazungu vilifuatilia vitendo vyao. Haraka, maafisa wa polisi wa ubaguzi wa rangi walishukiwa kuwaua.

Chunguzi mbili zlifanyika kati ya mwishoni mwa miaka ya 1980 na mapema miaka ya 1990. Lakini washukiwa hao hawakuwahi kufikishwa mahakamani. “Hakuna uchunguzi wowote uliowezesha kubaini wauaji,” imekumbusha Wizara ya Sheria. Familia zimekuwa zikidai kwa miaka mingi mwanga utolewe kwa matukio hayo.

Kulingana na mahakama, vielelezo vipya sasa vinawezesha uchunguzi kufunguliwa tena: "Wakati wa uchunguzi wa awali, familia na watu husika hawakusikilizwa. Ni wakati wa kurejesha imani katika mfumo wa mahakama", amesema Waziri Ronald Lamola, aliyenukuliwa katika taarifa.

Baada ya kuchaguliwa kwa Nelson Mandela mwaka 1994, Tume ya Ukweli na Upatanisho, iliyoongozwa na Askofu Mkuu Desmond Tutu, ilitoa msamaha kwa wale waliohusika na uhalifu wao. Lakini ilikataa kutoa msamaha kwa wauaji wa Cradock.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.