Pata taarifa kuu

DRC: Moïse Katumbi azuiwa kuondoka katika makazi yake kwa saa chache

Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mwanasiasa wa upinzani Moïse Katumbi alizuiwa kuondoka katika makazi yake kwa saa chache siku ya Jumatatu, Januari 8. 

Mgombea urais wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Moise Katumbi.
Mgombea urais wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Moise Katumbi. REUTERS - Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mmoja wa jamaa zake, wanajeshi waliojihami kwa silaha nzito walitumwa Jumatatu hii asubuhi karibu na nyumba yake katika kijiji cha Kashobwe, jimbo la Haut-Katanga, wakimzuia kuondoka nyumbani kwake. 

Tukio hilo limepatiwa suluhu mapema jioni. Gavana wa mkoa amelaani tukio hilo na kuamuru kuondolewa mara moja kwa kizuizi hicho. Kulingana na gavana huyo, hii ni "hatua mbaya" kwa upande wa polisi, iliyotumwa kwa mkoa huu kuwazuia baadhi ya watu kuharibu mali ya wapinzani wao wa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.