Pata taarifa kuu

Mwandishi wa habari wa Ufaransa amekamatwa nchini Guinea

Nairobi – Maafisa wa jeshi nchini Guinea wamemkamata mwandishi wa habari wa Ufaransa Thomas Dietrich, hatua inayokuaj wakati huu kukiwa na ripoti za kuzorota kwa uhuru wa vyombo vya habari katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Mwanahabari huyo alikamatwa alipokuwa akichunguza madai ya ufisadi katika kampuni ya kitaifa ya mafuta nchini humo (Sonap).
Mwanahabari huyo alikamatwa alipokuwa akichunguza madai ya ufisadi katika kampuni ya kitaifa ya mafuta nchini humo (Sonap). © Tenema DOUMBOUYA/ RFI MANDENKAN
Matangazo ya kibiashara

Mwanahabari huyo alikamatwa Jumapili katika mji mkuu, Conakry, alipokuwa akichunguza madai ya ufisadi katika kampuni ya kitaifa ya mafuta nchini humo (Sonap).

Vyanzo vya habari vinasema mwandishi huyo wa habari alikuwa anaangazia jinsi baadhi ya maofisa wa serikali ya mpito ya Guinea walivyopata utajiri wao na walikuwa nchini humo kwa siku kadhaa kuendeleza uchunguzi wao.

Si mara ya kwanza kwa  Dietrich kukamatwa nchini Guinea.

Mnamo Machi 2020, alikamatwa na kufukuzwa nchini humo baada ya kuwapiga picha maofisa wa polisi waliokuwa wakitekeleza oparesheni dhidi ya  maandamano ya upinzani katika mji mkuu Conakry.

Haijabainika iwapo Dietrich amefurushwa nchini kufuatia kukamatwa kwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.