Pata taarifa kuu

Uganda: Mzozo wa Gaza kujadiliwa kwenye mkutano wa 19 wa nchi zisizofungamana na upande wowote

Wawakilishi wa nchi 120 wanakutana hadi Januari 20 nchini Uganda, kwa ajili ya mkutano wa 19 wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa zinazoendelea kudai uhuru wao pamoja na mshikamano wao kuhusiana na migogoro ya kimataifa, ambayo ya hivi punde zaidi ni vita vya Gaza.

Muonekano wa Kampala, mji mkuu wa Uganda, ambako mkutano wa 19 wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na upande wowote unafanyika, kuanzia Jumatatu hii, Januari 15 (picha ya kielelezo).
Muonekano wa Kampala, mji mkuu wa Uganda, ambako mkutano wa 19 wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na upande wowote unafanyika, kuanzia Jumatatu hii, Januari 15 (picha ya kielelezo). AFP - YASUYOSHI CHIBA
Matangazo ya kibiashara

Ni mkusanyiko mkubwa zaidi wa viongozi wa dunia mjini Kampala kwa zaidi ya muongo mmoja kufuatia Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola mwaka 2007. Mamlaka ya Uganda haijagharimu gharama yoyote katika kuwapokea zaidi ya wajumbe 15,000 na wakuu wa nchi 28 wakiwemo viongozi wa Tanzania. Rwanda na Kenya, ambao wataanza kuwasili kuanzia Jumatano. Usalama umeimarishwa katika mji mkuu kwenye barabara kuu, randabauti na barabara zimekarabatiwa na kupambwa kwa maua. Juhudi ambazo pia zitatumika wakati wa kuandaa mkutano wa kilele wa nchi za Kusini na China, utakaofanyika siku ya Jumamosi kufuatia ule wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na upande wowote.

Haya ni mapinduzi ya uhakika kwa Rais Yoweri Museveni, anasema mchambuzi Timothy Kalyegira. "Kufanya mikutano miwili ya kilele katika wiki moja ni mafanikio," anabainisha. Afueni na mafanikio makubwa kwa mkuu wa nchi, anayekosolewa kwa sheria yake dhidi ya jamii ya wapenzi wa jinsia moja (LGBT( na kunyooshewa kidole cha lawama kwa rekodi yake ya haki za binadamu. "Mikutano hii miwili ya kilele inamruhusu Museveni kutoa changamoto kwa nchi za Magharibi," anaelezea Emmanuel Mutaizibwa, mhariri mkuu katika Nation Media Group. "Anatuma ujumbe wazi kwa ulimwengu: China na nchi za Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa zinamuunga mkono licha ya sera zake."

Utambuzi wa Wapalestina kwa hatua za kisheria za Afrika Kusini

Kama mnamo mwaka 2019, wakati wa mkutano wa mwisho huko Azerbaijan, swali la Palestina lilijumuishwa kwenye majadiliano. Riyad Mansour, Mwakilishi wa Kudumu wa Palestina katika Umoja wa Mataifa, amehimiza Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa kuunga mkono haki ya kujitawala ya watu wa Palestina: "Tutahitaji kuungwa mkono na harakati zetu baada ya kumaliza uchokozi huu ili kusaidia kumaliza uvamizi na kufikia haki zisizoweza kuondolewa za watu wa Palestina, pamoja na haki ya uhuru na haki ya kurudi kwa wakimbizi. "

Riyad Mansour pia ametoa shukrani zake kwa Afrika Kusini kwa malalamiko yake yaliyowasilishwa dhidi ya Israel huko Hague na kuitaka kundi la nchi hizo Zisizofungamana na upande wowote "kutowasahau" wraia wa Palestina. Nchi mwenyeji Uganda ni mojawapo ya nchi chache za Afrika kuwa na jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ambayo itaamua kama itakubali ombi la Pretoria.

Uhuru wa chakula na nishati

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Jenerali Jeje Odong, hapo awali alisisitiza umuhimu wa kufanya kazi pamoja ili kukabiliana na changamoto zinazoathiri nchi za Kusini. Kwanza kuna suala la biashara. Nchi nyingi za Kiafrika bado zinakabiliwa na matokeo ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na kushuka kwa kasi kwa bei za vyakula, hali ambayo ilisababihwa na  vita vinavyoendelea nchini Ukraine. Wataalam wanaaini kwamba kundi la nchi hizi Zisizofungamana na upande wowote zinapaswa kutetea uhuru bora wa chakula kwa nchi 120.

Pia wanatetea uhuru wa nishati ili kupunguza gharama za uzalishaji na hivyo kufanya nchi za Kusini kuwa na ushindani zaidi. njia, kulingana na wao, kupunguza utegemezi wa nchi za Kusini juu ya bidhaa na kupunguza madeni yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.