Pata taarifa kuu

Benin yapokea chanjo yake ya kwanza dhidi ya Malaria

Benin imetangaza kuwa imepokea dozi zake za kwanza za chanjo dhidi ya malaria siku ya Jumnne Januari 16, 2024, sababu kuu ya vifo vya watoto wachanga nchini humo. Mamlaka itaanza kuzitumia katika miezi ijayo.

Hatua hii imetajwa kuwa mafanikio katika vita dhidi ya malaria
Hatua hii imetajwa kuwa mafanikio katika vita dhidi ya malaria © UNICEF
Matangazo ya kibiashara

"Malaria bado ni janga na inawakilisha chanzo kikuu cha vifo vya watoto chini ya umri wa miaka 5 nchini Benin," Waziri wa Afya wa Benin Benjamin Hounkpatin ametangaza katika mkutano na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Cotonou, ambapo amepokea rasmi dozi 215,900 za chanjo ya RTS,S. . Chanjo za kwanza zitafanyika "ndani ya miezi michache", ameongeza.

Nchini Benin, 40% ya huduma ya wagonjwa wa nje na 25% ya waliolazwa hospitalini wanahusishwa na Malaria, kulingana na waziri. Chanjo iliyopokelewa inakusudiwa kuwachanja "takriban watoto 200,000" walio chini ya umri wa miaka miwili nchini humo, Faustin Yao, mtaalamu wa chanjo katika ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini ​​​​Benin, ameliambia shirika la habari la AFP, kulingana na ratiba ya chanjo ya dozi nne katika miezi 6, Miezi 7, miezi 9 na miezi 18.

Benin ni nchi ya tatu kupata dozi za chanjo ya Malaria baada ya Cameroon na Sierra Leone, kufuatia awamu ya majaribio iliyofanywa katika nchi za Ghana, Kenya na Malawi iliyoratibiwa na Shirika la Afya Duniani na kufadhiliwa na Vaccine Alliance (Gavi), Global Fund na Unitaid..

Zaidi ya watoto milioni 2 wamechanjwa katika nchi hizi tatu za Kiafrika, na kusababisha "kupungua" kwa vifo na kupungua kwa aina kali za Malaria na kulazwa hospitalini, Gavi inasema. Kulingana na shirika la Afya duniani, WHO, karibu kila dakika, mtoto wa chini ya umri wa miaka 5 hufariki kutokana na Malaria.

ugonjwa huu unaosababishwa na vimelea vinavyoenezwa na aina fulani za mbu, unasalia kuwa janga la kutisha kutokana na kuongezeka kwa upinzani wake kwa matibabu. Mnamo mwaka 2021, wagonjwa milioni 247walirekodiwa kote ulimwenguni, na wagonjwa 619,000 walifariki, kulingana na WHO, ambayo inabainisha kuwa ugonjwa huo huathiri zaidi bara la Afrika (95% ya wagonjwa na 96% ya vifo).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.