Pata taarifa kuu

Anthony Blinken ziarani Afrika kudumisha ushawishi wa Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anaanza ziara ya wiki moja katika pwani ya magharibi ya Afrika siku ya Jumatatu ili kudumisha ushawishi wa Marekani katika bara ambalo ushindani kutoka Beijing na Moscow ni mkubwa wakati ukosefu wa utulivu katika Sahel ukitia wasiwasi zaidi kuliko hapo awali.

Katika ziara hii ya Afrika Magharibi, Antony Blinken atasaidia nchi "katika nyanja zote kuimarisha jamii zao na kupigana dhidi ya upanuzi wa tishio la kigaidi ambalo tunashuhudia huko Sahel", anaelezea Molly Phee, naibu waziri anaehusika na Afrika ambaye alitembelea Niger mnamo mwezi wa Desemba.
Katika ziara hii ya Afrika Magharibi, Antony Blinken atasaidia nchi "katika nyanja zote kuimarisha jamii zao na kupigana dhidi ya upanuzi wa tishio la kigaidi ambalo tunashuhudia huko Sahel", anaelezea Molly Phee, naibu waziri anaehusika na Afrika ambaye alitembelea Niger mnamo mwezi wa Desemba. © Evelyn Hockstein / AP
Matangazo ya kibiashara

 

Mkuu wa diplomasia ya Marekani anaanzia ziara yake nchini Cape Verde, mshirika wa Marekani ambaye anasifu utulivu wa kidemokrasia wa visiwa hivi vinavyozungumza Kireno vyenye wakaazi nusu milioni.

Marekani imetoa kiasi cha dola milioni 150 kupitia programu mbili, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa bandari katika mji mkuu Praia, uboreshaji wa barabara na mfumo wa usambazaji maji ya kunywa. Mpango wa tatu wa msaada unajadiliwa. Kisha Bw. Blinken ataelekea Côte d'Ivoire, Nigeria na Angola.

Hii ni ziara yake ya kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara katika kipindi cha miezi kumi, wakati ambapo vita vya Ukraine na mzozo kati ya Israel na Hamas vinatawala habari za kimataifa.

Kuimarisha demokrasia

Katika ziara hii ya Afrika Magharibi, Antony Blinken atasaidia nchi "katika nyanja zote kuimarisha jamii zao na kupigana dhidi ya upanuzi wa tishio la kigaidi ambalo tunashuhudia huko Sahel", anaelezea Molly Phee, naibu waziri anaehusika na Afrika ambaye alitembelea Niger mnamo mwezi wa Desemba.

Pia atahimiza nchi kufanya "usalama wa raia wakati wa operesheni za kijeshi na kukuza haki za binadamu na maendeleo ya jamii" kuwa kipaumbele, ameongeza kwa vyombo vya habari.

Antony Blinken, anayezungumza Kifaransa vizuri na shabiki wa kandanda, anatarajiwa kuwasili Jumatatu jioni mjini Abidjan ambako Côte d'Ivoire inacheza mechi kali ya Kombe la Mataifa ya Afrika ambayo ni mwenyeji kwa sasa.

Nchini Côte d'Ivoire, Bw. Blinken atakaribisha uimarishaji wa demokrasia tangu Alassane Ouattara aingie madarakani mwaka wa 2011. Nchi hiyo imepata utulivu baada ya mgogoro mkubwa wa baada ya uchaguzi wa 2010-2011 ambao ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000. Ikipakana na Mali na Burkina, hadi sasa imefanikiwa kukomesha tishio la wanajihadi. Tukio la mwisho lililohusishwa na makundi yenye silaha kaskazini mwa nchi lilitokea mapema mwaka 2021.

Utawala wa Biden ulitangaza mwaka jana mpango wa miaka kumi wa kuhimiza utulivu na kuepuka migogoro katika nchi za Benin, Ghana, Guinea, Côte d'Ivoire na Togo, nchi za pwani ambazo ziko katika macho ya makundi ya jihadi. Ziara ya Bw. Blinken inajiri siku chache baada ya ile ya mwenzake wa China, Wang Yi, ambaye pia alitembelea Togo, Tunisia na Misri.

 

Beijing imekuwa ikifanya kazi kwa muda mrefu katika bara la Afrika, hasa kufadhili miundombinu katika nchi nyingi. Tangu ziara ya mwisho ya Bw. Blinken katika eneo hili mnamo mwezi wa Machi 2023, hali ya kisiasa imebadilika kwa kiasi fulani.

Wakati huo, alikwenda Niger kumuunga mkono rais mteule Mohamed Bazoum katika nchi hii ambapo Marekani ina wanajeshi zaidi ya elfu moja na vituo vya ndege zisizo na rubani kwa ajili ya mapambano dhidi ya wanajihadi. Lakini miezi minne baadaye, Bw. Bazoum alipinduliwa na mapinduzi ya kijeshi na utawala mpya unatafuta kubadilisha washirika wake: Wanajeshi wa Ufaransa wamefukuzwa na uhusiano unaimarika na Moscow.

Urusi imeendeleza ushawishi wake katika nchi kadhaa za Kiafrika zinazozungumza Kifaransa katika miaka ya hivi karibuni, hasa kwa uwepo wa kundi la wanamgambo wa Wagner katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na Mali na uhusiano na Burkina Faso.

Hali ya usalama katika Sahel bado inatia wasiwasi: Makundi ya kijihadi yenye mafungamano na Al-Qaeda au Islamic State bado yanafanya mashambulizi ya umwagaji damu katika nchi za Mali, Burkina Faso na Niger, nchi tatu zikiongozwa na wanajeshi walioingia madarakani wakati wa mapinduzi. Nchini Niger, Wamarekani kwa sasa wameweka kambi yao na wanajeshi wao lakini Washington inazingatia chaguzi nyingine, hasa katika nchi za pwani zenye utulivu zaidi.

"Maeneo kadhaa" yanachunguzwa kwa ajili ya kambi ya ndege zisizo na rubani, kulingana na maneno yaliyosemwa mwaka jana na Jenerali James Hecker, kamanda wa Jeshi la Wanahewa la Marekani kwa Ulaya na Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.