Pata taarifa kuu

Cameroon yazindua chanjo ya kimfumo dhidi ya malaria

Cameroon imezindua siku ya Jumatatu kampeni ya kwanza kimfumo na kwa kiwango kikubwa dhidi ya malaria, "hatua ya kihistoria" kulingana na shirika la Afya Duniani, WHO, katika kupambana na ugonjwa huu, moja magonjwa yanayosababisha vifo zaidi kati ya watoto wa Afrika.

Mtoto anapokea dozi ya chanjo ya Malaria nchini Burkina Faso.
Mtoto anapokea dozi ya chanjo ya Malaria nchini Burkina Faso. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

 

Noah Ngah, mtoto mchanga wa miezi sita, alipokea sindano yake ya kwanza ya chanjo ya RTS,S kwa kutiwa moyo na nyimbo za wauguzi katika hospitali ndogo katika mji wa Soa, kilomita 20 kutoka mji mkuu Yaoundé, moja ya vituo vingi vya chanjo katika “wilaya 42 zilizopewa paumbele” katika nchi hiyo kubwa ya Afrika ya Kati yenye wakaaji milioni 28 hivi.

"Ni siku ya kihistoria kidogo. Hadi sasa tulikuwa tumefanya utangulizi mdogo wa majaribio katika nchi 3 - Kenya, Ghana na Malawi - kuelewa jinsi ya kutumia chanjo. Huko Cameroon tunahamia moja kwa moja kwenye utangulizi wa kawaida" , amesema Aurélia Nguyen, mkurugenzi wa programu ya Gavi, Muungano wa Chanjo.

Malaria, ni ugonjwa unaoambukizwa kwa binadamu kwa kuumwa na aina fulani za mbu. Unaua zaidi ya watu 600,000 kila mwaka, 95% yao barani Afrika, kulingana na shirika la Afya Duniani (WHO). Na katika bara hili, watoto chini ya umri wa miaka 5 wanachangia zaidi ya 80% ya vifo.

"Kwa kweli ni hatua ya mabadiliko, tumekuwa tukifanya kazi ya chanjo ya malaria kwa muda mrefu sana, ilichukua miaka 30. Ni ugonjwa ambao ni mgumu sana kwa sababu unaambukizwa na vimelea wenye mzunguko wa maisha ambao ni ngumu sana. Tuna chombo ambacho kitaweza kuwa na manufaa kwetu, ambacho kina ufanisi ambao umeonyeshwa, ambacho kina usalama: ni chombo muhimu cha ziada", anaongeza Bi Nguyen.

Vipi kuhusu nchi nyingine za Afrika?

Uchaguzi wa Cameroon ulichochewa na ukweli kwamba ni nchi ambayo matukio ya ugonjwa huo ni ya juu sana. "Kwa hivyo tuliangazia Cameroon kwa sababu hapo ndipo chanjo itakuwa na athari chanya na tunazingatia haswa maeneo ya kijiografia ambayo matukio ni ya juu," kulingana na Aurélia Nguyen.

Zaidi ya dozi 300,000 za chanjo ya RTS,S dhidi ya malaria, kutoka kwa kundi la dawa la Uingereza GSK, la kwanza kuthibitishwa na kupendekezwa na WHO, zilipelekwa Cameroon mnamo Novemba 21. Ilichukua miezi miwili kuandaa kuanza kwa kampeni hii ambapo sindano ya kuzuia malaria inatolewa bila malipo, kulingana na serikali, na kwa utaratibu kwa watoto wote walio chini ya umri wa miezi sita, kwa wakati mmoja kama chanjo nyingine za lazima au zilizopendekezwa.

Mpango wa Gavi unahakikisha kuwa unafanya kazi ili kuanza kusambaza chanjo katika nchi nyingi iwezekanavyo. Nchi thelathini zimeonyesha nia.

"Tunatumai kuwa katika miaka miwili ijayo tutakuwa na utekelezaji mpana. Tutazingatia kwanza maeneo yaliyo hatarini na kisha kidogo tutaweza kupanua kulingana na kile ambacho nchi zinataka kufanya," anasema Aurélia. Nguyen.

Nchi nyingine tayari zimepata dozi na ziko katika mchakato wa awamu hii ya utekelezaji, maandalizi, mafunzo, kama vile Burkina Faso na Senegal. Nchi nyingine, nje ya Afrika, lakini ziko katika maeneo ya kijiografia ambapo vidudu vya kike vya Anopheles vya malaria vinaenea, na ambavyo vinastahiki usaidizi wa Gavi, vitastahiki programu sawa.

"Tunaona kwamba maeneo ya kijiografia ambayo mbu hawa wanaongezeka. Tunaona kwamba aina ya mbu inazidi kuwa pana. Kwa hiyo tunawaona India, tunawaona kusini mwa Ulaya, kwingineko Asia au Amerika ya Kusini, na hii ambapo nchi nyingine zinaweza kuwa na nia,” anasema mkurugenzi wa programu ya Gavi, Muungano wa Chanjo.

Gavi, Muungano wa Chanjo The Gavi Alliance in iliundwa mwaka wa 2000, inafanya kazi kutoa chanjo katika nchi zenye mapato ya chini. Ni ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi unaosaidia kuchanja zaidi ya nusu ya watoto duniani dhidi ya baadhi ya magonjwa hatari zaidi. Muungano huo unaleta pamoja serikali za wafadhili na nchi zinazopokea misaada, Shirika la Afya Duniani (WHO), UNICEF, Benki ya Dunia, sekta ya chanjo, mashirika ya kiufundi, mashirika ya kiraia na washirika kadhaa wa sekta ya kibinafsi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.