Pata taarifa kuu

Wanajeshi waliotoweka Pwani ya Somalia wamefariki: Jeshi la Marekani

Nairobi – Jeshi la maji la Marekani limetangaza kumalizika kwa zoezi la siku 10 la kuwatafuta na kuwaokoa maofisa wake wawili waliotoweka Pwani ya Somalia usiku wa tarehe 11 ya mwezi Januari.

Wanajeshi jao wamekuwa na jukumu la kuziua usafirishaji wa silaha katika Pwani ya Somalia
Wanajeshi jao wamekuwa na jukumu la kuziua usafirishaji wa silaha katika Pwani ya Somalia US Navy/ Cmdr Michael Junge
Matangazo ya kibiashara

Maofisa hao wa jeshi la maji la Marekani waliotoweka wakati wakijaribu kuizuia meli iliyokuwa imebeba silaha.

Mmoja wa wanajeshi hao aliripotiwa kuanguka kwenye maji kabla ya mwenzake kuruka ndani kwa jaribio la kumuokoa. Hakuna afisa alionekana tena baada ya tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamandi ya Marekani, baada ya kipindi cha siku 10 kuwatafuta maofisa hao, wamelazimika kuhitimisha zoezi hilo na kwamba hawajaweza kupatikana.Marekani inasema maofisa hao wamefariki

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa kwa sasa huenda maofisa hao wamefariki na hatua ya kuopoa miili yao imeanza.

Wanajeshi hao walikuwa sehemu ya kitengo kilichopewa majukumu ya kuzuia usafirishaji wa silaha katika pwani ya Somalia.

Uwepo wao kwenye eneo hilo hakujahusishwa na operation inayoendelea ya kulinda meli katika bahari ya shamu dhidi ya mashambulio ya waasi wa Houthi kutoka nchini Yemen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.