Pata taarifa kuu

Namibia: Chama tawala kinasema rais Geingob anaendelea kupokea matibabu

Nairobi – Chama tawala nchini Namibia Swapo, kimesema rais Hage Geingob yuko sawa kiafya na kwamba anaendelea kupokea matibabu yake dhidi ya saratani. 

Geingob amekuwa rais wa nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika tangu mwaka wa 2015
Geingob amekuwa rais wa nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika tangu mwaka wa 2015 AFP
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliopita, afisi ya rais ilitangaza kuwa rais Geingob ataanza matibabu ya saratani baada ya uchunguzi wa kimatibabu kubaini uwepo wa saratani kwenye mwili wake.

Licha ya kuthibitishwa kuwa mkuu wa nchi alikuwa na amepatikana na ugonjwa huo, afisi ya rais ilisema ataendelea na shughuli zake za kikazi kama kawaida, suala ambalo limethibitishwa na naibu wa chama chake Netumbo Nandi-Ndaitwah.

Aidha Ndaitwah ametoa wito kwa raia wa Nambia kumpa nafasi kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 kuendelea kupokea matibabu bila ya kutoa madai yasiokuwa na msingi.

Raia kwenye taifa hilo wanatarajiwa kushiriki uchaguzi wa urais na wabunge mwishoni mwa mwaka huu.

Geingob, ambaye amekuwa rais wa nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika tangu mwaka wa 2015, anamaliza muhula wake wa mwisho ofisini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.