Pata taarifa kuu

Ukoma: upatikanaji wa wagonjwa ni moja ya changamoto katika kutibu janga hili

Zaidi ya wagonjwa 20 hadi 25,000 hugunduliwa kila mwaka katika bara la Afrika pekee. Ukoma huathiri hasa maeneo yenye umaskini uliokithiri. Ni katika maeneo haya ambapo kunapatikana kesi mbaya zaidi za ugonjwa huu, hasa nchini Benin au Côte d'Ivoire, ambapo 25% ya watu walioathiriwa na ukoma wamepata ulemavu usioweza kurekebishwa. Upatikanaji wa wagonjwa ni changamoto kubwa.

Los primeros síntomas de la lepra aparecen en la piel.
Los primeros síntomas de la lepra aparecen en la piel. © C. Fohlen pour la Fondation Raoul-Follereau
Matangazo ya kibiashara

 

Vita dhidi ya ukoma barani Afrika ni ngumu zaidi kwa sababu ya matatizo matatu, anaeleza Dk Christian Johnson wa Wakfu wa Raoul-Follereau, akizungumza na Victor Cariou wa timu ya chumba cha habari cha RFI kanda ya Afrika.

"Kwanza, kuna shida ya kijiografia. Ni wagonjwa wanaoishi katika mbali kabisa, ninamaanisa, unapochukua gari, huwezi kufika, unapochukua pikipiki, huwezi vile vile kufika, kwa hiyo, lazima uendelee kwa miguu kwenda kijiji cha mbali zaidi.

Tatizo la pili ni usikivu wa kifedha katika mifumo yetu yote ya afya barani Afrika. Mgonjwa lazima alipe, na tuna shida ya watu wa vijijini, ni watu masikini. Na kwa sababu hiyo, tatizo hili la upatikanaji wa fedha husababisha kuchelewa kwa vipimo.

Mbali na upatikanaji huu wa kifedha, tuna tatizo la ufikiaji wa kitamaduni. Kwa wagonjwa wengi, wanasema ukoma ni kutokana na uchawi. Kwa hiyo, unapokuwa na dalili za ukoma, hatutaambiwa ‘nenda ukamwone mhudumu wa afya’, utakwenda kumwona mganga wa kienyeji na yote haya yataongeza muda kabla ya kugundulika. Haya ndiyo tunayoyaita matatizo ya kiuendeshaji, yaani leo hii bado tuna asilimia 25 ya wagonjwa wanaogundulika wakiwa wamechelewa  na hivyo kupata ulemavu. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.