Kongamano la Afrika- Italia linafanyika jijini Rome
Nairobi – Baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika wanakutana jijini Rome Italia, kuhudhuria kongamano la Afrika- Italia ambalo linalenga kuimarisha uhusiano kati ya Afrika na taifa hilo la bara Europa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Kwa mujibu waziri mkuu wa Italia, Giorgia Meloni , nchi yake inalenga kutumia mkutano huo wa kilele wa siku mbili kuzindua mbinu mpya ya kushirikiana na nchi za Afrika kwa manufaa ya pande zote.
Mojawapo ya sekta zinazotarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo ilikupata ushirikiano zaidi ni pamoja na nishati, maendeleo ya kiuchumi na miundombinu, utamaduni, usalama wa chakula, elimu na mafunzo yenye viwango vya juu.
Mkutano huo ulioanza Jumapili, unalenga pia kukuza uwekezaji katika nchi za Afrika kama mkakati wa kuzuia uhamiaji usio wa kawaida kutoka bara hilo kwenda barani Ulaya.
Mataifa mengine kadhaa yameandaa mikutano ya aina hiyo ili kuimarisha uhusiano na nchi za Afrika, zikiwemo Ujerumani, Urusi na China.