Pata taarifa kuu
UHARAMIA-USALAMA

Visa vya uharamia vyaongezeka pwani ya Somalia, katikati ya mgogoro katika Ghuba ya Aden

Jeshi la wanamaji la India lilitangaza mnamo Januari 29, 2024 kwamba liliokoa meli ya uvuvi ya Irani iliyotekwa nyara na maharamia wa Kisomali, shambulio la hivi karibuni la aina hii lilitokea katika Bahari ya Hindi, wakati ambapo waasi wa Houthi huko Yemen, wakiungwa mkono na Iran wanaendesha mashambulizi yao wenyewe katika Bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden.

Picha hii iliyotolewa na Jeshi la Wanamaji la India inaonyesha kikosi cha wanamaji ambao wamejihami kwa silaha wakiwa wamesimama nyuma ya maharamia 10 wa Kisomali waliokamatwa, mikono yao ikiwa imefungwa kamba, baada ya kuzuia jaribio la uharamia kwenye meli ya uvuvi yenye bendera ya Iran ya Al Naeemi katika pwani ya mashariki ya Somalia, Jumatatu Januari 29, 2024.
Picha hii iliyotolewa na Jeshi la Wanamaji la India inaonyesha kikosi cha wanamaji ambao wamejihami kwa silaha wakiwa wamesimama nyuma ya maharamia 10 wa Kisomali waliokamatwa, mikono yao ikiwa imefungwa kamba, baada ya kuzuia jaribio la uharamia kwenye meli ya uvuvi yenye bendera ya Iran ya Al Naeemi katika pwani ya mashariki ya Somalia, Jumatatu Januari 29, 2024. © Indian Navy via AP
Matangazo ya kibiashara

Je, kuna hatari ya kuzuka upya kwa uharamia katika pwani ya Somalia? Wakati mashambulizi ya waasi wa Houthi wa Yemen yameongezeka tangu kuzuka kwa vita huko Gaza katika jaribio la kukwamisha biashara na Israel, meli kadhaa zimekuwa zikilengwa katika Ghuba ya Aden. Meli tatu za uvuvi zililazimika kuokolewa katika siku za hivi karibuni baada ya mashambulizi ya maharamia.

Operesheni ya mwisho ya uokoaji ilizinduliwa Januari 29, 2024 na meli ya jeshi la wanamaji la India katika Ghuba ya Aden, karibu na pwani ya Somalia, kwa kuiokoa meli ya uvuvi iliyokuwa na wanamaji 19 wa Pakistani, na kuwakamata karibu maharamia kumi.

Mnamo Januari 27, wanajeshi wa India waliokoa meli nyingine ya uvuvi iliyotekwa nyara katika eneo hilo kwa kutoa msaada kwa wafanyakazi wa Irani waliochukuliwa mateka.

Siku hiyo, kikosi Maalum cha Wanamaji wa Ushelisheli na Walinzi wa Pwani pia walijibu ishara ya dharura, kusini, katika pwani ya Mogadishu, ambapo maharamia walikuwa wamechukuwa udhibiti wa meli ya Sri Lanka.

Matukio haya hayajatengwa katika miezi ya hivi karibuni, kutokana na mashambulizi yanayofanywa na waasi wa Houthi dhidi ya meli zinazohusishwa na Israel. Vikosi vya kimataifa vinavyoshika doria kwenye Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi vimerejea kwenye Bahari Nyekundu, na hivyo kupunguza kiwango cha ufuatiliaji katika maeneo ya kusini zaidi, na kuzua hofu ya kuongezeka kwa vitendo vya uharamia, ingawa idadi yao ilipungua zaidi tangu mwaka 2011 baada ya kuanzishwa ukaguzi wa kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.