Pata taarifa kuu

Zaidi ya wahamiaji 300 haramu warejeshwa Nigeria kutoka Libya

Chombo kinachohusika na kupambana na uhamiaji haramu nchini Libya, kwa uratibu na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), kimepanga siku ya Jumanne zoezi la kuwarejesha katika nchi yao Wanigeria 323 ambao ni wahamiaji haramu.

Libya, iliyoko umbali wa kilomita 300 kutoka pwani ya Italia, ni mojawapo ya nchi wahamiaji haramu, wengi wao kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara, wanoyotumia kwa kuanza safari yao hatari kuelekea Ulaya, kwa kutumia  njia ya bahari kwa kuhatarisha maisha yao.
Libya, iliyoko umbali wa kilomita 300 kutoka pwani ya Italia, ni mojawapo ya nchi wahamiaji haramu, wengi wao kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara, wanoyotumia kwa kuanza safari yao hatari kuelekea Ulaya, kwa kutumia njia ya bahari kwa kuhatarisha maisha yao. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

"Tumetekeleza siku ya Jumanne zoezi la kuwafurusha wahamiaji haramu 163, raia wa Nigeria kutoka uwanja wa ndege wa Mitiga (kaskazini-magharibi), wakiwemo wanawake 107, wanaume 51 na watoto watano," Jenerali Mohamad Baredaa, mkuu wa kitengo cha usalama katika chombo hiki kiliyo chini ya mamlaka ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Siku hiyo, "Wanigeria 160 watarejeshwa nchini mwao kutoka uwanja wa ndege wa Benina huko Benghazi" (kaskazini-mashariki), ameongeza.

Tangu makubaliano yaliyofikiwa mwaka wa 2023 kati ya mamlaka ya magharibi, kusini na mashariki, chombo kinachosimamia kinacosimamia zoezi la kuwarejesha makwao wahamiaji haramu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, yenye makao yake makuu mjini Tripoli (kaskazini-magharibi), kimefanya majaribio kwa njia ya kuratibu. Wakiwa wamevalia nguo nyeusi na kofia kichwani, raia wa Nigeria, wengi wao wakiwa wanawake, walikusanyika kwenye chumba cha kusubiri, wakipewa vitafunio na pasi, kabla ya kupanda mabasi kuelekea uwanja wa ndege.

Libya, iliyoko umbali wa kilomita 300 kutoka pwani ya Italia, ni mojawapo ya nchi wahamiaji haramu, wengi wao kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara, wanoyotumia kwa kuanza safari yao hatari kuelekea Ulaya, kwa kutumia  njia ya bahari kwa kuhatarisha maisha yao. Wasafirishaji na wasafirishaji haramu wametumia fursa ya hali ya ukosefu wa utulivu ambayo imetawala nchini Libya tangu kuanguka na kifo cha dikteta wa zamani Muammar Gaddafi mwaka 2011 kuendeleza mitandao safari hizi haramu.

Zaidi ya wahamiaji 700,000 wapo katika ardhi ya Libya, kulingana na IOM, kulingana na data iliyokusanywa kati ya mwezi Mei na Juni. Mnamo 2015, IOM ilianzisha mpango wa "kuwarejeshaa kwa hiari" wahamiaji na wakimbizi wanaotaka kuondoka Libya. Mnamo mwaka 2023, watu 9,370 walipokea usaidizi kutoka kwa IOM ili kurejea kwa hiari katika nchi zao za asili, baada ya wahamiaji 11,200 mnamo 2022, kulingana na tovuti ya IOM.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.