Pata taarifa kuu

Jeshi la Umoja wa Afrika lakamilisha awamu ya pili ya kuondoka nchini Somalia

Kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (Atmis), ambacho kinashiriki katika mapambano dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali Al Shabab, kilitangaza Ijumaa kuwa kimekamilisha awamu ya pili ya kuwaondoa wanajeshi wake, yaani wanjeshi 3,000, zoezi ambalo limechelewa kwa miezi minne kulinana na ratiba iliyopangwa awali.

Baada ya kuondoka kwa wanajeshi 5,000 katika awamu mbili za kwanza, karibu wanajeshi 14,600 kutoka Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya na Uganda wapo nchini.
Baada ya kuondoka kwa wanajeshi 5,000 katika awamu mbili za kwanza, karibu wanajeshi 14,600 kutoka Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya na Uganda wapo nchini. © Hassan Ali ELMI / AFP)
Matangazo ya kibiashara

 

Serikali ya Somalia iliomba "kusitishwa kwa zoezi la Umoja wa Afrika kuwaongoa wanajeshi wake kwa sababu za kiufundi" kwa muda wa miezi mitatu, zoezi ambalo lilipangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba, baada ya kupata "vikwazo kadhaa" dhidi ya wapiganaji wa kundi la Kiislamu lenye uhusiano na al-Qaeda ambalo limekuwa likiongoza uasi kwa zaidi ya miaka 16 katika nchi hii katika Pembe la Afrika.

"Misheni ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (Atmis) ... imekamilisha awamu ya 2 ya uondoaji, ambayo ilihusisha kupunguzwa kwa askari 3,000. Atmis imehamisha vituo saba vya operesheni kwa serikali ya shirikisho ya Somalia na kufunga vingine viwili," alitangaza katika taarifa.

Baada ya kuondoka kwa wanajeshi 5,000 katika awamu mbili za kwanza, karibu wanajeshi 14,600 kutoka Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya na Uganda wapo nchini. Kulingana na ratiba iliyopigiwa kura katika azimio la Umoja wa Mataifa, kikosi hiki cha "mpito" lazima kikamilishe zoezi lake la kuondoa waajeshi wake mwishoni mwa mwaka 2024 na kukabidhi usalama wa nchi kwa wanajeshi na polisi wa Somalia.

"Hivi karibuni tutaanza maandalizi ya awamu inayofuata, Awamu ya 3, yenye lengo la kupunguza nguvu za askari wetu kwa askari 4,000 mwezi Juni. Nina imani katika mafanikio yetu ya kuendelea kulingana na mtazamo wetu wa umoja na madhubuti," Jenerali Sam Okiding, Kamanda wa Atmis, amesema katika katika taarifa. Iliyowekwa rasmi mnamo Aprili 1, 2022. Atmis ilichukua nafasi kutoka kwa Amisom, iliyoundwa mnamo 2007 kusaidia serikali ya Somalia katika kukabiliana na uasi wa Al Shabab. Kutoka kwa mamlaka ya awali ya miezi sita, Amisom ilidumu miaka 15.

Ingawa ilifurushwa nje ya miji mikuu mwaka 2011-2012, Al Shabab bado imeanzishwa katika maeneo makubwa ya vijijini, hasa katikati na kusini mwa nchi, ambako mara kwa mara hufanya mashambulizi dhidi ya malengo ya usalama, kisiasa na kiraia.

Serikali ya Rais Hassan Cheikh Mohamoud ilijihusisha mwezi Agosti, pamoja na wanamgambo wa koo na usaidizi wa mashambulizi ya anga kutoka kwa kikosi cha Umoja wa Afrika (Atmis) na Marekani, katika mashambulizi makubwa katikati mwa nchi, ambayo yalifanya uwezekano wa kutwaa tena maeneo makubwa. Lakini maendeleo haya yalikwama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.