Pata taarifa kuu

Somalia: Kikosi cha AU kinatarajiwa kuondoka kufikia mwishoni mwaka huu

Nairobi – Ujumbe kutoka Umoja wa Afrika ambao umekuwa ukizuru Somalia kwa siku tano, umethibitisha kuwa kikosi cha AU kinatarajiwa kuondoka nchini humo kufikia mwishoni mwaka huu.

AU imesema kuwa itahakikisha kwamba hakuna mwanya wa kiusalama wakati kikosi cha ATMIS kitakapoondoka
AU imesema kuwa itahakikisha kwamba hakuna mwanya wa kiusalama wakati kikosi cha ATMIS kitakapoondoka AP - Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa ujumbe huo Alhaji Sarjoh Bah, anayehusika na masuala ya utatuzi wa mizozo, siasa na amani kwenye Umoja huo, amesema, AU itahakikisha kuwa hakuna mwanya wa kiusalama wakati kikosi cha ATMIS kitakapoondoka.

Kufikia mwezi Juni, awamu ya tatu ya kikosi hicho kuendelea kuondoka, itaendelea ambapo wanajeshi 4,000 watarudi nyumbani.

Kikosi cha ATMIS kinatarajiwa kuachia wanajeshi wa Somalia, kazi ya kuendelea kulinda hali ya usalama wa ndani kufikia Desemba 31 mwaka huu kama ilivyokuwa imeratibiwa.

ATMIS kiliundwa Aprili 1 mwaka 2022 baada ya jina kubadilishwa kutoka AMISOM ili kuanza mchakato wa mpito kuanza kukabidhi kazi za kiusalama kwa jeshi la Somalia, baada ya kikosi cha wanajeshi 22,000 kutoka nchini Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya na Uganda.

Tangu mwaka 2007 kikosi hicho kimekuwa na kazi ya  kuwalinda raia na kupambana kundi la kigaidi la Al Shabab ambalo limekuwa likitishia kuchukua serikali jijini Mogadishu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.