Pata taarifa kuu

Congo-Brazzaville: AU yatoa wito wa kukomesha 'kuingilia' maswala ya ndani ya Libya

Wito wa kusitishwa kwa "uingiliaji" wa nchi za kigeni katika mgogoro wa Libya umezinduliwa Jumatatu huko Brazzaville, kufuatia mkutano wa Kamati ya Ngazi ya Juu ya Umoja wa Afrika (AU) kuhusu nchi hii ya Afrika Kaskazini inayokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu 2011.

Raia wa Libya walikusanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Tripoli wakiandamana kuunga mkono serikali ya Waziri Mkuu Abdel Hamid Dbeibah, Septemba 24, 2021.
Raia wa Libya walikusanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Tripoli wakiandamana kuunga mkono serikali ya Waziri Mkuu Abdel Hamid Dbeibah, Septemba 24, 2021. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu, wa tisa tangu kuundwa kwa kamati hii ya AU inayoongozwa na mkuu wa nchi ya Kongo Denis Sassou Nguesso, umeandaliwa kama utangulizi wa mkutano wa maridhiano kati ya Walibya uliopangwa kufanyika Aprili 28 huko Sirte, katika ardhi ya Libya.

"Wajumbe wa Kamati wamethibitisha kuunga mkono mchakato wa kisiasa unaoongozwa na Libya, ambao unalenga kuendesha uchaguzi mkuu utakaowezesha kuunganisha serikali," inabaini taarifa ya mwisho iliyosomwa na Jean-Claude Gakosso, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo.

Tangu kuanguka kwa kiongozi Muammar Gaddafi, aliyeuawa wakati wa uasi mwaka 2011, Libya, iliyoathiriwa na ghasia na migawanyiko ya kindugu, imekuwa ikitawaliwa na serikali mbili hasimu: mmoja huko Tripoli (Magharibi), ikiongozwa na Abdelhamid Dbeibah na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa. nyingine katika Mashariki, ikiwa na Bunge na kuhusishwa na kambi ya Marshal Haftar, ambayo ngome yake iko Benghazi.

"Nguzo ya upatanisho"

Wakati wa ufunguzi wa kesi hiyo, rais wa Kongo Denis Sassou Nguesso, amekumbuka kuwa "kila mara alipendelea mazungumzo jumuishi kati ya Walibya kama kichocheo cha maridhiano na sharti la mchakato wa uchaguzi". "Hakuna mpango utakaokuwa na nguvu zaidi kuliko ule unaotoka kwenye mioyo na akili za Walibya wenyewe. Wakati wa vita umekwisha bila shaka," ameongeza, akielezea vita vya Libya kama "janga".

Moussa Faki Mahamat, mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, pia amesisitiza kuwa "mgogoro wa Libya umedumu kwa muda mrefu na kugharimu maisha ya watu wake." Kulingana na Moussa Faki Mahamat, vita imechochea "ugaidi katika Sahel" na matokeo yake "katika suala la uharibifu wa kisiasa na ukosefu wa utulivu". Kulingana na AU, mgogoro wa Libya ni wa pande nyingi: kijeshi, usalama, kisiasa, kitaasisi, kiuchumi na kifedha.

Mbali na Sassou Nguesso na Faki Mahamat, wameshiriki hasa katika mkutano wa Brazzaville rais wa sasa wa AU, rais wa Comoro Azali Assoumani, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Abdoulaye Bathily na mwenyekiti wa Baraza la Urais la Libya Mohammed el-Menfi

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.