Pata taarifa kuu

Senegal: Mahakama imechapisha orodha mpya ya wagombea urais iliyoboreshwa

Nairobi – Mahakama ya kikatiba ya Senegal, hapo jana imechapisha orodha mpya ya wagombea urais iliyoboreshwa, ambapo kiujumla haikuwa na mabadiliko sana isipokuwa kuondolewa kwa jina ma mmoja wa wagombea aliyetangaza kujiondoa kwenye kinyanganyiro hicho.

Hata hivyo haifahamiki ikiwa rais Salla atatangaza tarehe nyingine hivi karibuni
Hata hivyo haifahamiki ikiwa rais Salla atatangaza tarehe nyingine hivi karibuni © AFP/Seyllou
Matangazo ya kibiashara

Wadadisi wa mambo wanasema uamuzi wa mahakama hii umelenga kujaribu kuzima wito wa wadau wa uchaguzi wakiwemo wanasiasa wa upinzani, waliotaka mchakato mzima wa baraza la kikatiba kuwapata wagombea hao kumulikwa.

Tangu kutolewa kwa orodha hiyo ambayo haikujumuisha wagombea vinara kama Ousmane Sonko aliyeko jela na Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani Abdoulaye Wade, kuliibua maswali na madai ya rushwa kwenye mahakama hiyo.

Katika tarifa yake, mahakama hiyo imesema hakukuwa na uwezekano wa kufanya uchaguzi katika tarehe iliyokuwa imepangwa awali, lakini ikatoa wito kwa mamlaka zinazosimamia uchaguzi, kuufanya mapema iwezekanavyo siku chache tangu ikatae tangazo la rais Sall.

Kwa majuma kadhaa sasa, nchi ya Senegal imeshuhudia maandamano yaliyogeuka vurugu baada ya tangazo la rais Macky Sall kuahirisha uchaguzi uliokuwa ufanyike mwishoni mwa juma hili na bunge kupitisha ufanyike mwezi Desemba, hatua iliyopingwa vikali.

Hata hivyo haifahamiki ikiwa rais Salla atatangaza tarehe nyingine hivi karibuni, wakati huu upinzani ukishinikiza uchaguzi ufanyike kabla ya muhula wa sasa kukamilika April 2 mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.