Pata taarifa kuu

Senegal: Wafungwa 400 wa kisiasa wameachiwa huru

Nairobi – Waziri wa masuala ya haki nchini Senegal Aissata Tall Sall ametangaza kuachiwa huru kwa karibia waandamanaji 400 wa kisiasa kutoka jela.

Waandamanaji hao walikamatwa na kufungwa gerezani wakati wa maandamano ya mwezi Machi mwaka wa 2021 na mwezi Juni 2023
Waandamanaji hao walikamatwa na kufungwa gerezani wakati wa maandamano ya mwezi Machi mwaka wa 2021 na mwezi Juni 2023 AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji hao walikamatwa na kufungwa gerezani wakati wa maandamano ya mwezi Machi mwaka wa 2021 na mwezi Juni 2023.

Licha ya tangazo hilo, waziri Sall hakuweka wazi iwapo mwanasiasa wa upinzani Ousmane Sonko pamoja na mgombea wa urais Bachirou Diomaye Faye wataachiwa huru.

Serikali inasema hatua hiyo inalenga kupunguza joto la kisiasa kwenye taifa hilo
Serikali inasema hatua hiyo inalenga kupunguza joto la kisiasa kwenye taifa hilo © AFP - SEYLLOU

Aidha waziri huyo ameeleza kuwa hatua hiyo ya kuwaachia huru kwa wafungwa hao wa kisiasa imelenga kupunguza joto la kisiasa kwenye taifa hilo.

Maandamano ya kisiasa nchini Senegal yamekuwa yakifuatiwa na ripoti za watu kukamatwa na polisi, vifo pia vikithibitishwa kutokea.

Maandamano ya hivi punde yalifanyika baada ya kuhairishwa kwa tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwezi huu
Maandamano ya hivi punde yalifanyika baada ya kuhairishwa kwa tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwezi huu REUTERS - ZOHRA BENSEMRA

Hivi karibuni, watu watatu walithibitishwa kufariki wakati wa maandamano ya kupinga kuhairishwa kwa uchaguzi mkuu wa tarehe 25 ya mwezi Februari.

Baada ya tangazo hilo, kiongozi huyo amesema uchunguzi unaendelea kubaini waliokuwa nyuma ya maandamano ya vurugu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.