Pata taarifa kuu

Senegal: Rais Macky Sall kuhutubia bunge hii leo

Nairobi – Rais wa Senegal, Macky Sall, hivi leo anatarajiwa kuhutubia taifa kwa mara nyingine ambapo huenda akatangaza tarehe mpya ya uchaguzi, wakati huu wanasiasa wa upinzani wakimtuhumu kwa kujaribu kuchelewesha mchakato mpya wa uchaguzi.

Mack Sall- Rais wa Senegal
Mack Sall- Rais wa Senegal © AP/Christophe Ena
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati huu wagombea tofauti kwenye uchaguzi huo wakitaka kufanyika kwa uchaguzi wa urais mara moja, kauli hiyo ikija wakati huu vuguvugu la kiraia linalojiita Aar Sunu Election au kulinda uchaguzi wetu, likitangaza maandamano mapya siku ya Jumamosi kushinikiza kufanyika kwa uchaguzi huo.

Aidha, wagombea hao wanaendelea kusisitiza kuwa uchaguzi huo, ufanyike kabla ya Aprili tarehe 2, wakati muhula wa rais Sall utakapomalizika.

Wanasisitiza kuwa baada ya Mahakama ya Katiba kufuta hatua ya rais Sall kuahirisha uchaguzi huo, wanapendekeza kuwa, uchaguzi huo ufanyike tarehe tatu mwezi Machi.

Maandamano ya kupinga kuhairishwa kwa uchaguzi wa urais yalishuhudiwa jijini Dakar
Maandamano ya kupinga kuhairishwa kwa uchaguzi wa urais yalishuhudiwa jijini Dakar AFP - JOHN WESSELS

Katika hatua nyingine, Mahakama ya kikatiba jana imechapisha orodha mpya ya wagombea urais iliyoboreshwa, ambapo kiujumla haikuwa na mabadiliko sana isipokuwa kuondolewa kwa jina la mmoja aliyetangaza kujiondoa kwenye kinyanganyiro hicho.

Wadadisi wa mambo wanasema uamuzi huo  umelenga kujaribu kuzima wito wa wadau wa uchaguzi wakiwemo wanasiasa wa upinzani, waliotaka mchakato mzima wa baraza la kikatiba kuwapata wagombea hao kuchunguzwa baada ya wanasiasa maarufu wa upinzani, Ousmane Sonko aliyeko jela na Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani Abdoulaye Wade, kuondolewa kwenye orodha ya wagombea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.