Pata taarifa kuu

Guinea: Amadou Oury Bah ameteuliwa kuwa waziri mkuu mpya

Nairobi – Nchini Guinea, kiongozi wa kijeshi Jenerali Mamady Doumbouya, amemteua Amadou Oury Bah, kuwa waziri Mkuu mpya, wiki moja baada ya kuivunja serikali.

Amadou Oury Bah, ndiye waziri mkuu mpya wa Guinea
Amadou Oury Bah, ndiye waziri mkuu mpya wa Guinea www.ufdg2010.org
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la kuteuliwa kwa Bah, mwanauchumi, ambaye sasa ataunda serikali mpya, limekuja wakati kukiwa na mgomo kwa siku ya pili ambao, ulikwamisha shughuli za kawaida jijini Conakry.

Maandamano hayo yanashinikiza kupunguzwa kwa bei ya vyakula, kuachiwa huru kwa  Sekou Jamal Pendessa, kiongozi wa vyama vya wafanykazi nchini humo pamoja na kulalamikia kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya Habari.

Baada ya kuunda serikali mpya, waziri mkuu mpya anatarajiwa kukubaliana na changamoto zinazowakabili wananchi wa taifa hilo, ikiwa ni pamoja na kuimarisha mazingira ya utendaji kazi wa watumishi wa umma.

Msemaji wa muungano wa wafanyakazi nchini humo Amadou Diallo, amesema wanasubiri kuona iwapo serikali mpya itakayoundwa itatekeleza kikamilifu malalamishi yao, kabla ya kusitisha mgomo ambao wiki hii umesababisha watu wawili kuuawa kwa kupigwa risasi na maafisa usalama jijini Conankry.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.